HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 8, 2017

NISHATI MBADALA NI SULUHISHO LA KUPUNGUZA UKATAJI MITI OVYO- AFRI TEA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Ikiwa ni katika kuboresha mazingira na kuepukana kutaka miti zipo njia nyingi sana za kuhakikisha mazingira yanaendelea kutunzwa na kuboreshwa, Kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders imekuja na suluhisho la kuachana na masuala ya ukataji miti ovyo.

Watanzania wametakiwa kubadilika kwa kuacha kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa bali watumie nishati mbadala ambayo itasaidia katika kutunza mazingira.

Hayo yamesemwa wakati akizungumza na Globu ya Jamii, Mkuu wa Masoko na Biashara wa Afri Tea and Coffee Blenders (ATCB)Zachy Mbenna amesema wamekuja na njia mbadala ya kuepukana na matumizi ya mkaa kwa kutengeneza nishati mbadala inayotengenezwa kwa mabaki ya miti (magome) aina ya miwati.

Mbenna amesema, utumiaji wa magome hayo katika utengenezaji wa nishati mbadala umechukua nafasi ya ukataji miti hai ambapo watu wanatumia kutengeneza mkaa na kupelekea kuharibu mazingira.

"Nishati hiyo mbadala ambayo inajulikana kama Briquets inatengenezwa kwa magome ya mabaki ya miti ya miwati ambayo inatumika kwa ajili ya kutengenezea ngozi, tulifikia hatua hii ya kutengeneza hizi baada ya kuona tunatumia zaidi ya tani nyingi zaidi za kuni ndani ya mwezi mmoja kitu ambacho kilikuwa kinatugharimu sana,"amesema Mbenna.

"Baada ya kuona tumefanikiwa katika kupunguza gharama pamoja na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni, baadhi ya viwanda navyo kutumia bidhaa hizi tukaamua kupeleka kwa wananchi kwa matumizi ya nyumbani ikiwemo pamoja na kuja na majiko yao maalumu kwani Briquets zinahitaji hewa ili kuweza kufanya kazi kwa uharaka zaidi, "amesema Mbenna.

Ametoa wito kwa makampuni, taasisi na watu wengine watambue wao ndiyo watu wa kwanza wa kulinda mazingira na njia nzuri ni kutumia nishati mbadala ambayo ni njia bora ya kuhifadhi mazingira.
Mkuu wa Masoko na Biashara wa kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders (ATCB) akielezea mkaa na aina ya majiko yanayotumika kwa nishati mbadala (Briquets) zinazotengenezwa kampuni ambapo yanapatikana kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Masoko na Biashara wa kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders (ATCB) akionyesha  mkaa na aina ya majiko yanayotumika kwa nishati mbadala (Briquets) zinazotengenezwa kampuni ambapo yanapatikana kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es salaam.
Fundi wa majiko yanayojulikana kama Simba Stones akielezea namna nishati mbadala ya mkaa wa magome ya miti (Briquets) inavyofanya kazi kwnye majiko hayo yanayopatikana  kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es salaam.
Fundi wa majiko yanayojulikana kama Simba Stones akielezea kwa wananchi waliojitokeza katika banda lao namna nishati mbadala ya mkaa wa magome ya miti (Briquets) inavyofanya kazi kwnye majiko hayo yanayopatikana  kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad