HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 14, 2017

MSHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA

Mshabiki wa Sunderland Bradley Lowery (6) amezikwa leo na mamia ya mashabiki wa timu hiyo pamoja na wachezaji wa Sunderland wakionyesha masikitiko makubwa kwa kuondokewa na moja ya mashabiki wao wakubwa.


Bradley  alifariki Ijumaa wiki iliyopita baada ya kuugua saratani kwa muda.ambapo katika uhai wake alikuwa mshabiki mkubwa wa timu ya Sunderland na ilifikia kipindi baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na Jermain Defoe kwenda kumjulia hali katika hopsitali aliyokuwa amelazwa.



Mchezaji Jermain Defoe, ambaye aliunda urafiki wa karibu sana na Bradley, aliungana na familia ya mvulana huyo kumuaga kwa mara ya mwisho.

Ibada ya wafu ilifanyika katika kanisa la Mtakatifu Yusufu kijijini mwao, wengi wakimsifu sana mvulana huyo kwa ukakamavu wake na sifa alizojilimbikizia.Bradley alikuwa anaugua ugonjwa ambao kwa Kiingereza hufahamika kama neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18.

Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.

Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.

Bradley alipewa matibabu lakini saratani yake ikaibuka tena mwaka jana. Wahisani walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea sana na haingeweza kutibiwa.

Wazazi wake Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham, waliambia Desemba kwamba alikuwa amesalia na "miezi kadha tu ya kuishi".Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli.Bradley alipendwa na maelfu ya watu na alipokea kadi 250,000 za kumtakia heri wakati wa Krismasi mwaka jana, kutoka kwa watu mataifa ya mbali kama vile Australia na New Zealand.


Habari kwa hisani ya BBC Swahili.

 Aliyekuwa Kocha wa Sunderland David Moyes katika msiba wa Bradley Lowery.
Ujumbe wa Bradley ukiwa umewekwa katika moja ya barabara

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad