HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 19 July 2017

MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU RTO PWANI AONDOLEWE

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimuuliza maswali Dereva wa basi la Safari Express lifanyalo safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (wapili kushoto) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwauliza maswali abiria wa basi la Safari Express lifanyalo safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kufanya ukaguzi wa magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi, Jonathan Shana, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (wapili kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani, Abdi Isango (wapili kushoto) katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na waendesha bodaboda wa Mji wa Chalinze, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, Chalinze na Bagamoyo mkoani Pwani. Masauni aliwataka waendesha boda boda hao kufuata sheria za barabarani na pia alimuagiza Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (wapili kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiwa katika ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi cha Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani ambapo alifanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) mkoani humo katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kufuata maelekezo aliyowahi kupewa ya kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) wakati alipokua anazungumza na askari wa usalama barabarani katika eneo la Sanzale, Bagamoyo. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Mabasi Kibaha, Chalinze pamoja na kukagua barabara hadi kufika mjini Bagamoyo.

Na Felix Mwagara (MOHA)
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Masauni akiwa ameambatana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu, alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha Maili Moja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo, kwa ajili ya kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka jana.
“Mwaka jana nilipofanya ziara kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna mapungufu katika ukaguzi wa magari, tukakubaliana atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo, lakini hakuna mabadiliko yoyote, magari hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria,” alisema Masauni na kuongeza kuwa;
“RTO ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya kinidhamu, hatutati uzembe, hatutaki kucheza na maisha ya watanzania.”
Masauni mara baada ya ukaguzi wa kituo hicho, aliendelea na ziara yake mkoani Pwani ambapo alifanya ukaguzi wa aina hiyo mjini Chalinze na baadaye Msata na kuimalizia ziara yake Bagamoyo.
Akiwa mjini Chalinze, Masauni alizungumza na waendesha bodaboda na kuwapa maelekezo kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani kwa kutobeba mishikaki, uvaaji wa kofia ngumu na pia kufuata sharia zote za usalama barabarani. 
“Mmenihakikishia kwa wale ambao hamkua na kofia ngumu kuwa mkitoka hapa mtakwenda kuzitafuta, hakikisheni mnafanya hivyo kwa usalama wenu pamoja na abiria mnaowabeba, ipendeni kazi yenu kwa kuheshimu sharia za usalama barabarani,” alisema Masauni. 
Akiwa njiani kuelekea Chalinze mpaka Bagamoyo, Masauni ambaye gari yake ilitolewa namba zinazomtambulisha nafasi yake (NWMNN), na kuweka namba za kawaida ili kujua kama akiendesha kwa mwendokasi barabarani matrafiki watalisimamisha gari lake, hata hivyo askari wa usalama barabarani sehemu kubwa hawakuwepo barabarani na pia waliokuwepo hawakuweza lisimamisha gari lake.
Kutokana na hatua hiyo, Masauni akagundua kuwa kuna uzembe mkubwa unaofanywa na matrafiki mkoani humo kwa kutofanyakazi zao kwa umakini, na kwa uzembe huo ndio chanzo cha ajali zinazotokea barabarani mara kwa mara.  
Akizungumza na matrafiki wilayani Bagamoyo ambao walifanya uzembe huo, aliwataka wabadilike haraka iwezekanavyo kufuata wajibu wao, na pia alitoa siku tatu kuhakikisha wanawakamata waendesha bodaboda wote ambao wanavunja sheria za usalama barabarani, na pia baada ya operesheni hiyo apewe ripoti haraka iwezekanavyo, na muda wowote atafanya ziara ya kushtukiza kuona kama maelekezo hayo wameyafanyia kazi.
“Bodaboda nimeziona nyingi zinapita hapa zikiwa zinavunja sheria, madereva na abiria hawajavaa kofia ngumu, na nyie mpo hapa mnaziangalia, sasa nawaagiza mtekeleze maagizo niliyotoa na pia sio nyie tu bali nchi nzima wahakikishe wanayakagua magari pamoja na bodaboda, na atakaepuuza atutacheka nae, tutapambana nae,” alisema Masauni.
Kwa upande wake Kamanda Msilimu, alisema ameyapokea maagizo yote na atahakikisha anayafanyia kazi ipasavyo kwa kuwasimamia matrafiki wote nchini kwa umakini mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad