HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 26 July 2017

Mama Salma Kikwete awapongeza BAKITA

Balozi wa Kiswahili Tanzania, Mama Salma Kikwete amelipongeza Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) na kampuni ya uchapishaji Longhon ya nchini Kenya kwa kazi kubwa ya kutunga Kamusi Kuu ya Kiswahili.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili jijini Nairobi Nchini Kenya, Mama Salma ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa ithibati hiyo iwe ni ushahidi wa kukubalika kwa Kamusi hiyo kwa matumizi rasmi katika nchi hizo mbili.
“Kama Balozi wa Kiswahili kwenye Bara letu la Afrika. Ni kazi kubwa sana ya kutunga kamusi ya Kiswahili na kuiwezesha kupata itifaki ya taasisi zinayosimamia kiswahili katika nchi zote mbili yaani Tanzania na Kenya,” alisema Mama Salma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad