HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 6 July 2017

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AKUTANA NA TIMU YA WATAALAMU KUTOKA BENKI YA DUNIA KUJADILI MASUALA YA WAKIMBIZI

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mpango wa Kuzisaidia Nchi Zilizoathirika na kuhifadhi Wakimbizi, waliofika wizarani kujadili masuala mbalimbali ya wakimbizi.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kiongozi wa timu ya Wataalamu kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mpango wa Kuzisaidia Nchi zilizoathirika na Kuhifadhi Wakimbizi, Joanna De-Berry (wakwanza kulia), akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira.Wataaalamu hao walifika wizarani kujadili masuala mbalimbali ya wakimbizi.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa wizara,jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke, akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,baada ya  timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mpango wa Kuzisaidia Nchi Zilizoathirika na kuhifadhi Wakimbizi kutembelea  wizara wakiwa na lengo la  kujadili masuala mbalimbali ya wakimbizi.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Mpango wa Kusaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi,Dk.  John Jingu, akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,baada ya  timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mpango wa Kuzisaidia Nchi Zilizoathirika na kuhifadhi Wakimbizi kutembelea  wizara wakiwa na lengo la  kujadili masuala mbalimbali ya wakimbizi.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiagana na Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumuia Wakimbizi(UNHCR),Joan Allison baada ya  timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mpango wa Kuzisaidia Nchi Zilizoathirika na kuhifadhi Wakimbizi kumaliza kikao  kilichojadili  masuala mbalimbali ya wakimbizi.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa wizara , jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mpango wa Kuzisaidia Nchi Zilizoathirika na kuhifadhi Wakimbizi, waliofika wizarani kujadili masuala mbalimbali ya wakimbizi.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa wizara , jijini Dar es Salaam.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad