HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 17 July 2017

KANUNI ZA ZA MATUMIZI YA DRONE KUANDALIWA –TCAA

 Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
NDEGE zinazorushwa bila rubani kwa ajili ya kupiga picha (Drone) ni marufuku kutokana na usalama wa anga.

Hayo aliyasema Mwanasheria wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Maria Memba wakati semina ya waandishi ya wa habari iliyofanyika mjini Morogoro, alisema  ndege hizo zinatakiwa kuwekewa kanuni kutokana na usalam.

Amesema wanaomiliki kwa sasa wasizitumie mpaka utaratibu  utakapo toka  ni pamojana kujua wanaomiliki ndege hizo na jinsi ya kuzitumia. Maria amesema ni ndege ndogo zinaaadhari kubwa kama zinaweza kukutana na  ndege  nyingine angani na kuweza kusababisha ajali ndege.

Aidha amesema kuwa utaratibu utatoka na wadau wanaomiliki ndege hizo kuelimishwa katika masuala ya usalama kanuni zake kutungwa kwa mujibu wa sheria. Maria amesema masuala ya anga ni mapana na kila siku teknolojia zinabadilika katika matumizi ya anga hivyo inawapasa kwenda na teknolojia hiyo.
 Mwanasheria Mwandamizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Maria Makalla  (kushoto) akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari juu ya majukumu ya Mamlaka hiyo, pamoja na matokeo ya ukaguzi wa Kimataifa walivyokaguliwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) wakati wasemina iliyofayika mkoani  Morogoro.
 Meneja  Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), BestinaMagutu  (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya majukumu ya Mamlaka hiyo, pamoja na matokeo ya ukaguzi wa Kimataifa walivyokaguliwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) wakati wasemina iliyofayika mkoani  Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa habari toka waliohudhuria semina ya majukumu ya  TCAA pamoja na matokeo ya ukaguzi wa Kimataifa walivyokaguliwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) wakati wa semina iliyofayika mkoani  Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo iliyofayika mkoani Morogoro kwa kuandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad