HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 19 July 2017

KAGERA SUGAR WAWEKA KAMBI DAR KWA MAANDALIZI YA MSIMU MPYAKikosi cha timu ya Kagera Sugar kimeweka kambi katika Jiji la Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti.


Kocha mkuu wa timu hiyo Mecky Mexime amejumuisha kikosi cha zamani na wale wa watakaoungana na wenzao katika kuimarisha timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya.

Katika sura mpya za kikosi cha Kagera Sugar ni Juma Nyoso aliyekuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka miwili kutokujihusisha na soka, Omary Daga na Abdala Mguhi kutoka African Lyon iliyoshuka daraja. Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .
Dakatri wa timu ya Kagera Sugar akiganga mchezaji aliyeumia katika  mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .

Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .

Kocha wa timu ya Kagera Sugar Mecky Mexime akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wanaoendelea na mazoezi katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es salaam.Picha na Globu ya Jamii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad