HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 19 July 2017

Hali ya Yusuf Manji bado tete, kesi yake yapigwa kalenda hadi mwezi ujao.


Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeambiwa, Mfanyabiashara, Yusufali Manji (41) bado anaumwa na yuko kwenye matibabu katika hospitali ya keko.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga amedai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa.

Amedai kuwa, kesi hiyo leo ilikuja kwa kutajwa lakini Upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena Agosti 4, mwaka huu.

Katika kesi hiyo, Manji anashtakiwa na wenzake watatu ambapo wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa.

Katika Mashtaka hayo, wanadaiwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya milioni 195.5 na mihuri ya JWTZ na magari ya serikali kinyume cha sheria..

washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali watu wa kampuni ya Quality Group Deogratius Kisinda(28), mtunza stoo Abdallah Sangey(46) na Thobias Fwere (43) mkazi wa Chanika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad