HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 24 July 2017

ESRF YAENDESHA WARSHA YA FURSA KATIKA UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA

WATANZANIA wameshauriwa kuchangamkia fursa za ufugaji wa samaki kibiashara kutokana na kuwepo kwa soko kubwa la bidhaa hiyo huku mnyororo wake wa thamani ukiwa na uhai mrefu kisekta. 
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bwana Amon Manyama wakati akifunga warsha ya siku moja juu ya ufugaji wa samaki kibiashara iliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na watu takribani 400. 
Bw. Manyama alisema kwamba watanzania wasipotumia fursa ya ufugaji wa samaki baada ya miaka mitano watakuwa wamepoteza fursa hiyo adimu inayoshawishi viwanda vidogo na vya kati. Alisema kimsingi yeye anaamini sekta ya ufugaji wa samaki ni viwanda tosha kutokana na muingiliano wake huku watu wakinufaika na minofu pia kuna ngozi na magamba ambayo yanakazi kubwa ya kutengeneza urembo, viatu na kadhalika. 
Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Margareth Nzuki akitambulisha wageni na malengo ya warsha ya fursa za ufugaji Samaki kibiashara.
Warsha hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)- Kitengo cha Maarifa na Ubunifu ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)- Idara ya Sayansi ya Wanyama, Ukuzaji Viumbe Majina Nyanda za Malisho, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) - Kikosi cha Kambi la Rwamkoma pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ilifunguliwa na Bi. Ritha Maly Kaimu Mkurugenzi Idara ya maendeleo ya viumbe wa majini. 

Akifungua warsha hiyo, Bi Ritha aliwashukuru waandaaji wa warsha hii kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa samaki "Warsha hii imekuja wakati muafaka ambapo uhitaji wa samaki umeongezeka sana ukiambatana na changamoto za upatikanaji wa samaki wa kutosha hivyo uwepo wa fursa hizi zitakazowasilishwa leo zitakua hakika ni mkombozi mkubwa kwa kukuza uzalishaji wa samaki nchini na kufungua fursa za biashara ya samaki kwa kufanya ufugaji huu kibiashara." alisema. Makamu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Hai Majini wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ritha Maly akisoma hotuba ya kufungua warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara.

Akielezea madhumuni na lengo la kufanya washa hii, Mkuu wa Kitengo cha Maarifa na Ubunifu (ESRF) Bi. Margareth Nzuki, alisema warsha hii ni mwendelezo wa warsha nyingine ambazo zinalenga kuwaelimisha wananchi fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na uvuvi ambazo tukitumia teknojia za kisasa zinaweza kuongeza kipato na kujenga uchumi, Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na watu mbalimbali waliojitokeza katika mafunzo hayo wakiwamo wafugaji na wanaotaka kuanza kufuga, alisema amefurahishwa na mahudhurio na kusema ameona ishara kubwa ya dhamira ya kufanya mapinduzi makubwa katika eneo la ufugaji wa samaki kwa kuwa tayari kutafuta maarifa juu ya ufugaji samaki kibiashara. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akisoma hotuba ya ukaribisho katika warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara.

Alisema Taasisi ya ESRF baada ya kufanya utafiti na kuwa na matokeo iliamua kuitisha warsha hiyo ili kwa mara nyingine tena kuopeleka faida ya kivitendo kwa wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi na kusukuma mbele gudurumu la maendeleo. "Taasisi yetu imekuwa msitari wa mbele kufanya tafiti mbali mbali ambazo kwa hakika zimekuwa na faida na matokeo makubwa kwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Kufuatia tafiti mbalimbali, msukumo na muitikio mkubwa wa jamii umeonekana katika maeneo mbali mbali ikiwemo pia ufugaji wa samaki." alisema Dkt. Kida na kuongeza kuwa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali imefanya tafiti juu ya fursa mbali mbali zinazoweza kutokea kutokana na ufugaji samaki. Afisa Mifugo wa Kituo cha Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi cha Bagamoyo, Emmanuel Maneno akitoa wasilisho la kwanza kuhusu Ufugaji wa Samaki katika Mabwawa.

 Warsha hii ilikuwa na mada mbalimbali ambazo ziliwakilishwa na wataalam waliobobea katika sekta ya ufugaji wa samaki. Katika mada mbalimbali washiriki walisisitizwa kuwa makini na kutohemka na kuhakikisha kwamba wanwatumia wataalamu hasa kupata mafunzo kabla ya kuingia katika shughuli za ufugaji. Akizungumzia ufugaji wa samaki katika mabwawa (pond fish farming),Bwana Emmanuel Maneno wa Kituo Cha Ufugaji Samaki Mbegani - Idara Ya Ukuzaji Viumbe Majini, alisema kwamba wataalamu wa serikali na wale wa halmashauri hufanyakazi ya upembuzi wa maeneo bure suala ni kuwafikisha katika eneo huisika ili aweze kuangalia eneo na kukushauri aina ya bwawa. Mkurugenzi wa Nuru Farm, Gloria Kavisheakitoa wasilisho kutoka kwa mfugaji kuhusu Ufugaji wa Samaki katika Mabwawa.

 Aidha mmoja wa wafugaji anayefanya ufugaji kibiashara kwa ufugaji mkubwa (large scale) kutoka Ruvu Farm, Bwana Nkhumbo Kantenga alizungumzia changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo katika ufugaji wa kibiashara lakini akisema kwamba kila changamoto inatolewa ufumbuzi na kwamba shamba lake linauza pia vifaranga na vyakula vya kuku. Pia Bi. Gloria Kavishe wa Nuru Farm mfugaji mdogo (small scale) alitoa uzoefu wake katika ufugaji wa samaki kibiahsara akihimiza watu wajiunge na biashara ya samaki kwa kuwa inalipa. Katika mada ya ufugaji katika vizimba mada ilitolewa na Luteni Kelvin Ngondo kutoka Jeshi la Kujenga Taifa – Kambi ya Rwamkoma, ufugaji huu unaonekana zaidi katika maeneo ya bahari na maziwa kwa kuwa unafaida nyingi mfano mfugaji kama atawafuga samaki wake kwa kufuata kanuni zote za ufugaji ana hakika ya kuwavuna samaki wengi wenye viwango bora. Kizimba kimoja kinaweza kuchukua samaki hadi elfu 5. Pia husaidia kuwaondoa uvuvi haramu lakini pia unatoa uwapo wa makundi ya ushirika ambayo yanaweza kusaidia kupata nafuu katika ulinzi na pia katika uwingi wa idadi ya samaki. Meneja wa Ruvu Farm, Nkhumbo Kantenga akitoa wasilisho kutoka kwa mfugaji mkubwa kuhusu Ufugaji wa Samaki katika Mabwawa.

Mtaalamu kutoka SUA Dkt. Nazael Madalla alizungumzia kwa undani namna ya kulisha samaki, uandaaji wa vyakula vyake na pia kujibu maswala muhimu kuhusu magonjwa na mana bora ya kupunguza gharama za chakula ili kuweka faida juu. Dkt. Gratian Bamwenda, Mtafiti Mshiriki wa ESRF, alitoa mada iliyohusu muingiliano wa ufugaji wa samaki kibiashara na masoko ya samaki. Alisema utunzaji na uhifadhi mzuri wa samaki baada ya kuvuliwa unasaidia sana kupata soko zuri la bidhaa hiyo. Alitoa mifano mbalimbali ya kutunza samaki ili kumsaidia mfugaji wa samaki kupata soko la uhakika. Luteni Kelvin Ngondo kutoka kikosi cha Jeshi la Wananchi 822 Rwamkoma cha Butiama, Mara akiwasilisha akitoa wasilisho kuhusu ufugaji wa samaki katika vizimba.

Licha ya mada mbalimbali za kuelimisha zilizotolewa na wakufunzi, washiriki walipata nafasi kumsikiliza Ofisa kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Bwana Marko Samson ambaye aliwahakikishia washiriki wa warsha kwamba benki hiyo ipo wazi kwa elimu na pia kwa kupata mitaji. Pamoja na wananchi zaidi ya 400 kufika kutafuta utaalamu wa namna ya kufuga huku wakioneshwa video, pia wanawarsha walipewa angalizo la utafutaji wa masoko ya uhakika kabla ya ufugaji kwani ni hatari kuanza kufuga ukiwa hujui soko liko wapi. Afisa Uvuvi wa Samaki kutoka SUMA JKT, Luteni Joseph Lyakurwa akitoa wasilisho la ufugaji samaki katika matanki. Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Wanyama, Ukuzaji viumbe maji na Nyanda za malisho wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Dk. Nazael Madalla. Mtafiti Mwenza wa ESRF, Dk. Gratian Bamwenda akitoa wasilisho kuhusu masoko ya bidhaa za samaki. Afisa Mwandamizi anayeshughulikia na kuendeleza wakulima wadogo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Marco Samson akieleza jinsi benki hiyo inavyowasaidia wakulima na wafugaji wadogo kukuza biashara zao. Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama akifunga warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara. Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya ESRF, Margareth Nzuki wakimpa maelezo mgeni rasmi kwenye warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara, Makamu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Hai Majini wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ritha Maly kuhusu ufugaji samaki wa kwenye matanki. Baadhi ya washiriki wa warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara wakipewa maelezo kuhusu ufugaji samaki wa kwenye matanki. Picha juu na chini ni Baadhi ya washiriki wa warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Margareth Nzuki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad