HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 13, 2017

DK. KIGWANGALLA AANZIA ZIARA YAKE YA KIKAZI MKOANI MTWARA, AHIMIZA WATUMISHI WA AFYA KUIMARISHA UZALENDO

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla ahimiza watumishi wa wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzingatia sheria, miongozo,  taratibu na maelekezo yao ya kazi.

Akiwa katika ziara hiyo Mkoani Mtwara, alielekeza watumishi hao kuwa dhamana waliyopewa kuwahudumia wananchi wenzao ni kubwa hivyo hawana budi kuzingatia kanuni za Afya ili kuepuka maambukizi yatakayotokana na uzembe .

Aliwataka kulipa kipaumbele suala la usafi wa mazingira, vifaa na maeneo yote wanayofanyia kazi hususan uhifadhi wa taka za hospitali katika utaratibu maalum unaozingatia  mfumo wa kinga na udhibiti wa taka  (Infection Prevention and Control) .

Miongoni mwa mambo mengine aliyoyabaini katika ziara hiyo ni ubovu wa baadhi ya vifaa tiba katika maabara na vyumba vya upasuaji na kuagiza katibu mkuu wizara ya Afya kuchunguza mikataba yote ya usambazaji vifaa tiba na matengenezo.

 Aidha, Dk. Kigwangalla alibaini baadhi ya vifaa vya kisasa vilivyomo katika vituo hivyo havitumiki ipasavyo kwasababu watumishi waliopo hawana ujuzi wa kuvitumia na alimwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa kulishughulikia tatizo hilo haraka sana kwa kuwajengea uwezo wataalam hao.

Mbali na kujionea hali hizo, Dk. Kigwangalla pia alitoa maagizo mbalimbali kwa watendaji wa vituo na viongozi wa Wilaya husika kuhakikisha wanasimamia ipasavyo utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Dk. Kigwangalla akiwa mkoani Mtwara, aliweza kutembelea katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali, kati hizo ni:  Kituo cha Afya Mahurunga, Kituo cha Afya Nanguruwe, Zahanati ya Kijiji cha Dinyecha.

Pia ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Newala na Kituo cha Afya Newala DC, Zahanati ya Lulindi, Zahanati ya Nagaga, Hospitali ya Halmashauri ya Masasi-Mkomaindo na Zahanati ya Mbonde.
Aidha, ameendelea na ziara yake Mkoani Ruvuma ambayo  atatatembelea vituo vya Afya na Hospitali za Mkoa huo.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi na wa Hospitali ya Wilaya ya Masasi-Mkoamaindo (Hawapo pichani). Wengine anayemfuatia ni Mbunge wa Jimbo la Masasi  Mh. Abdalla Chuachua na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msasi. 
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua kitanda maalum cha upasuaji alichokikuta katika hyali ya kutoridhisha kiafya.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Newala, Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake hiyo ya kukagua mambo mbalimbali ya kiutendaji katikaa hospitali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad