HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 18, 2017

BAKWATA YAITAKA SERIKALI KUMCHUKULIA HATUA MTU MMOJA ANAYEJIITA MTUME MKOANI PWANI.

 Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata ,Sheikh Khamis Said  akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, juu ya Vyombo vya Dola kuchukua hatua stashiki kwa  mtu mmoja mkazi wa Mkoa wa Pwani, Hamza Issa  anaejiita Nabii IIyasa .

Waandishi wa Habari wakimsilikiliza  Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata, Sheikh Khamis  Said, leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.



Baraza la ulamaa limetoa wito kwa vyombo vya dola kumchukulia hatua stahiki mtu aliyejitokeza katika mkoa wa pwani na kudai yeye ni Mtume.

 Akisoma wito huo, kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally,  Mwenyekiti wa Halmashauri kuu Bakwata Sheikh Hamisi Said Mataka amesema, anachodai mtu  huyo aliyetajwa kwa jina la Hamza Issa kuwa yeye ni nabii hayako kabisa katika mafundisho ya kiislamu.



Amesema kauli ya Issa kudai yeye ni mtume na kisha na kwamba ni muislamu na kutumia maandiko ya uislamu ni upotoshaji mkubwa ambao ukiachwa bila kudhibitiwa ni kuruhusu fujo na uvunjifu wa amani.




"Kwa mujibu wa maelezo yaliyoenea katika mitandao ya kijamii na ya kutoka baraza za Masheikh wa Mkoa wa Pwani chini ya kiongozi wake Sheikh na Qadhi wa Mkoa wa Pwani, amedai kuwa yeye ni Nabii Ilyasa kwa maana ya kwamba roho ya Nabii Ilyasa imemuingia yeye Hamza Issa na kwa hiyo yeye wamekuwa Nabii Ilyasa" amesema Sheikh 

Ameongeza maelekezo na mafundisho ya uislamu yako wazi kuwa hakuna Mtume mwingine katika Uislamu baada ya Mtume Muhammad (S.A.W) na kwamba upatikanaji wa MTU ndani ya uislamu na kudai kuwa yeye ni Mtume ni kutaka kuamsha hisia Kali za waislamu nchini.



"Baraza la Ulamaa linapenda kuwafahamisha waislamu kwamba, yeyote atakayemfuata mpotoshaji huyu atakuwa ametoka ndani ya uislamu" amesema Sheikh Mataka.


Pia Baraza limetoa wito kwa Masheikh wa Mikoa, Wilaya na viongozi wa taasisi mbali mbali za Kiislam kutotoa fursa ya aina yoyote kwa huyo anayejiita Nabii ( Hamza Issa), ili kuzuia kuipotosha jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad