HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 28 July 2017

BAADA YA KUTAMBIANA, NUSU FAINALI YA PILI YA SPRITE BBALL KINGS KUENDELEA KESHO DON BOSCO OYSTERBAY

Manahodha wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Michuano ya mpira wa kikapu ya Sprite Bball Kings 2017 imezidi kupamba moto baada ya timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kutambiana.

Michuano hiyo inayoendelea wikiendi hii katika Viwanja vya Don Bosco imekuwa ya ushindani mkubwa ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili ya nusu fainali.

Manahodha kutoka timu hizo wametambiana kwa kila mmoja kumuambia mpinzani wake kuwa ajipange katika mchezo huo wa raundi ya pili ambapo matokeo hayo yanaweza kutoa majibu ya kuelekea fainali.

Kwa upande wa timu ya mpira wa kikapu ya Mchenga Bball Stars, nahodha wao Mohamed Yusuph amesema kuwa watahakikisha mchezo wa pili dhidi ya wapinzani wao Flying Dribblers unamalizika kwa siku hiyo kwani hawatakubali kuona wanaenda raundi ya tatu.

Nahodha wa Flying Dribblers Geofly lea ametamba na kuwatahadharisha Mchenga kuwa hawatakubali kuona wanarudia makosa ya mchezo uliopita kwani katika raundi hii watahakikisha ushindi utakuwa upande wao.

Kwa upande wa wapinzani wengine Timu ya Kurasini na TMT, Nahodha wa Kurasini Rajab Hamis amewatahadharisha TMT kuwa raundi hii wamejipanga sana na wataumaliza mchezo siku hiyo huku nahodha wa TMT Isihaka Masoud akiweka wazi kuwa alama walizofungwa ni chache sana lazima wapindue matokeo.

Hatua hiyo ya nusu fainali ilianza kupigwa mwishoni mwa wiki iliyopita na tayari Flying Dribllers walikubali kipigo cha vikapu 119 dhidi ya 70 kutoka kwa Mchenga All Stars na Kurasini waliibuka na ushindi wa vikapu 87 kwa 80 vya TMT.

Nusu fainali ya pili itaendelea wikiendi hii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad