HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 14 July 2017

Apewa tuzo kwa kutunza sokwe vizuri

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe  Profesa Maghembe akizungumza wakati wa hafla ugawaji wa tuzo kwa Dk. Jane Goodall ambaye ametoa mchango mkubwa kwenye sekta ya uhifadhi na kubainisha tabia za sokwe ambazo watu wengi hawazijui. Profesa Maghembe aliongeza kuwa mtafiti huyo ambaye ni raia wa Uingereza amebainisha katika tafiti zake kwamba sokwe wana fikiri na wana hisia kama walivyo binadamu. Picha zote na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi akitoa machache wakati wa hafla ya ugawaji wa tuzo kwa Dk. Jane Goodall ambaye ni muhifadhi Wanyama aina ya Sokwe aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60.
Dkt. Jane Goodall, ambaye aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama aina ya Sokwe kwa miaka 60 akitoa shukrani za pekee. Wageni waalikwa waliofika kuhudhuria hafla hiyo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia), akimkabidhi Tuzo ya Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe, Dkt. Jane Goodall, aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60 katika hifadhi mbalimbali na baadaye kujikita katika Hifadhi ya Gombe. Dkt. Jane Goodall akionyesha cheti chake cha kutambua mchango wake katika Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe. Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, akimkabidhi Tuzo ya Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe, Dkt. Jane Goodall, aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60 katika hifadhi mbalimbali na baadaye kujikita katika Hifadhi ya Gombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, George Waitara na Bi. Gertude Mongella.

 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
 Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Hifadhi za Tanzania TANAPA, limempatia tuzo nne za Heshima, mwanasayansi na mtafiti wa kimataifa Dkt. Jane Goodall. Dkt. Jane amekabidhiwa tuzo mapema leo na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Magembe ambazo ni kinyago cha Sokwe, Kitenge, cheti cha heshima na ngao. Tuzo hiyo ya heshima imetolewa maalumu kwa kutambua mchango wake katika masuala ya utafiti na uhifadhi wa Sokwe kwenye hifadhi ya taifa ya Gombe ambao ameufanya kwa zaidi ya miaka 60. Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo, Waziri wa Magembe amesema, Tanzania ni nchi ya kwanza ya uhifadhi katika bara Africa. Katika hifadhi zetu za taifa za wanyama mbali mbali ambazo ziko 16, ziko pia, hifadhi za taifa mbili, Gombe na Mahale ambazo wanyama wanaohifadhiwa humo kwa sehemu kubwa ni Sokwe ambapo hata katika dunia hizo mbili ndio hifadhi nzuri kupita zote. Amesema, Kazi kubwa iliyofanywa na mtafiti huyo imeiwezesha jamii kugundua kuwa, Sokwe, wanajitambua na kushirikiana. Wao kama wanyama, wana hisia zao kama viumbe na kama binadamu. Amesema, kabla ya utafiti huo wa Sokwe, na katika ulimwengu wa sayansi binadamu ndio waliokuwa wa wanahisiwa kuwa ndio wenye hisia na kushirikiana kama viumbe wenye akili sana kumbe hata Sokwe kwani wao pia wanatumia nyenzo katika maisha yao. Ameongeza kuwa tafiti anazofanya zimekusanya takwimu zenye maana kubwa sana katika uhifadhi wa Sokwe na pia katika uhifadhi wa wanyama pori. "Kwa mchango wake huu alioutoa, kidunia, kimataifa lakini kwa Tanzania kutoa mchango huu, tumeamua kumtunukia tuzo katika uhifadhi wa wanyamapori na zaidi Sokwe" amesema Waziri Maghembe. Ameongeza, uharibifu wa mazingira unatokana na ukosefu mkubwa wa elimu, kabla ya Sokwe kufanyiwa utafiti huu uliofanywa, tulikuwa tunajua sisi binadamu ni tofauti na Sokwe,kumbe katika vinasaba vyetu kama binadamu asilimia 99 ni sawa sawa na Sokwe, tofauti ni moja asilimia moja tu, ya ubongo wetu na uwezo wetu ndio mkubwa kuliko wao, mambo mingine yote tuko sawa sawa", amesema Magembe. Aidha Waziri amesisitiza kuwa, msimamo wa Serikali katika utafiti huu mgumu uliofanywa na Dkt. Jane ni kuendeleza kazi hizo, kupanua taasisi ya utafiti ya wanyama hao kama binadamu na kuileta iwe na ushirikiano na mashirika ya wanyama pori nchini kama Tanapa, Ngororo na mengineyo na kuhakikisha kazi ya utafiti inaendelea na kutufanya tuzidi kuwa viongozi duniani katika sekta hiyo. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kikazi amesema, Tanapa ina kila sababua ya kumpa tuzo ya Heshima, Dkt, Jane kwani amekuwa akitumia muda wake mwingi sana kufanya utafiti na kuwapatia taarifa za kutosha zinazowawezesha kujua mienendo na tabia za wanyama aina ya Sokwe ambao unaweza kuwapata kwenye hifadhi ya Gombe iloyopo Kigoma na kwenye Milima ya Mahale pekee. Amesema taarifa hizo zinaisaidia Tanapa kuweka mikakati sahihi juu ya namna ya kusimamia hifadhi ya Gombe na kuwasimamia Sokwe ambao wako katika hatari ya kutoweka, kwani bila taarifa hizi, kungekuwa na uwezekano wa idadi ya wanyama hao kuwa ndogo kuliko sasa ambao wanakadiriwa kuwa zaidi ya 80. Pia Dkt. Jane amesaidia kutoa mafunzo na kuwawezesha wafanyakazi wa Tanapa kihakikisha Sokwe wanasimamiwa inavyopaswa. "Idadi ya wanyama walioko ndani ya hifadhi inaonekana inaongezeka lakini pia kama wanyama wanaoonelana kuwa wanaishi kwenye mazingira yao ya asilo wao huwa hawatambui mpaka iliyopo, wamekuwa na tabia ya kutoka na maeneo yaliyopo nje ya hifadhi mengi yameharibiwa na wamekuwa wakiuwawa kwa mambo mbali mbali, lakini tunafanya jitihada kuhakikisha tunaweka mifumo sahihi hata wakiwa nje ya hifadhi', amesema Kikazi. Kwa upande wake Dkt. Jane ameishukuru sana Serikali ya Tanzania na Tanapa kwa kutambua mchango wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad