HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 4, 2017

Airtel na DTBi wazindua maabara ya kompyuta kwa wanafunzi wa Dar kujifunza kutengeneza programu


  Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa maabara ya Kompyuta itakayojulikana kama“Airtel Fursa Lab” ili kufundisha watoto na vijana mafunzo ya TEHAMA chini ya usimamizi na ushirikiano kati ya Airtel na Dar Teknohama Bussiness Incubator (DTBI)  kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano na Mkurugenzi Mkuu wa DTBI Eng. George Mulamula (kushoto). “Airtel Fursa Lab” imezinduliawa leo kwenye shule ya msingi ya kijitonyama iliyoko wilaya ya Kinondoni.
 Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora (wapili kulia) akikata utepe ili kuzinduzia  maabara ya Kompyuta ya “Airtel Fursa Lab” ili kufundisha watoto na vijana mafunzo ya TEHAMA chini ya usimamizi na ushirikiano kati ya Airtel na Dar Teknohama Bussiness Incubator (DTBI)  kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano na Mkurugenzi na kushoto kwake ni Mkuu wa DTBI Eng. George Mulamula na Mwenyekiti wa kamisheni ya ICT Tanzania Maharage Chande na Mweyekiti wa Bodi ya Shule ya msingi Kijitonyama John Mutajwaha “Airtel Fursa Lab” imezinduliawa leo kwenye shule ya msingi ya kijitonyama iliyoko wilaya ya Kinondoni.
 kushoto ni Mwanafunzi wa shule ya msingi  Aghakan Serira Telerico akielezea jinsi alivyotengeneza program ya Robot  kwa Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora wakati alipozindua Maabara hiyo  kwenye shule ya msingi ya kijitonyama wilaya ya kinondoni, wanaoshudia ni Mkuu wa DTBI Eng. George Mulamula na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano ambao ndio wasimamizi na wadhamini wa  Maabara hiyo. “Airtel Fursa Lab” imezinduliwa leo kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama na kukuza ujuzi katika maswala ya kitechnolojia
Mwanafunzi wa shule ya msingi  Aghakan mzizima Brayan Basimaki (wakwanza kushoto) akielezea jinsi anavyotengeneza program zake za kompyuta  kwa Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora wakati alipozindua Maabara hiyo  kwenye shule ya msingi ya kijitonyama wilaya ya kinondoni, Maabara hiyo. “Airtel Fursa Lab” imezinduliwa leo kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama na kukuza ujuzi katika maswala ya kitechnologia.

Dar es Saalam, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) leo imezundua maabara ya kompyuta ilijulikanayo kama  “Airtel Fursa Lab” katika shule ya msingi ya kijitonyama wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama na kukuza ujuzi katika maswala ya kitechnologia
  
Maabara hiyo ya “Airtel Fursa Lab” itatoa mafunzo ya msingi ya kompyuta kwa hatua ya awali  na mafunzo ya hatua ya juu zaidi kwa  wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, chuo kikuu na jamii nzima kwa ujumla. Walimu pia watapata mafunzo ya kompyuta yatakayowawezesha kutoa msaada kwa wanafunzi watakaotumia maabara hiyo

Akizindua maabara hiyo mgeni rasmi ambaye ni  Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Faustin Kamuzora aliwapongeza Airtel na DTBi kwa kuweka nguvu pamoja  katika ushirikiano huu ambao utachochea mapinduzi kwa vijana wa kitanzania katika sekta ya habari namawasiliano (ICT).  Hii itasaidi kujenga jamii yenye msukumo wa kutafuta masuluhisho na kujiongezea wigo katika ujasiliamalia ambayo utasaidia kukuza uchumi wa viwanda kwa taifa”

Pia alitoa wito kwa wadau wengine kuunganisha nguvu katika ushirikiano kama huo ili kuleta maendeleo zaidi”

Akiongea katika uzinduzi huo pia, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya alisema “ wakati Tanzania imejipanga kufikia uchumi wa viwanda mahitaji ya wafanyakazi wenye ueledi katika teknologia wanahitajika sana ili kufikia malengo haya. Hivyo ni muhimu kujenga vijana wenye ujuzi  na ueledi wakiwa katika umri mdogo na hivyo tunajisikia fahari kuwa sehemu ya kutoa ujuzi na kukuza maendeleo ya watanzania katika Teknologia ya Tehama kupitia maabara ya Airtel Fursa  tunayozindua leo.

Maabara ya Airtel Fursa ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutumia teknologia ya mawasiliano ya simu pamoja na Tehama katika kustawisha biashara na kukuza ujuzi katika teknologia  na hivyo kuwa na nguvukazi yenye ueledi zaidi.  Natoa wito kwa vijana na jamii nzima kuchangamkia fursa hii na kuitumia maabara hii ya kompyuta ipasavyo. Aliongeza Mallya

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George Mulamula alisema “Tanzania tuna changamoto katika kutoa mafunzo kwa vitendo  ili kuchochea na  kuendeleza ubunifu wa teknolojia itakayoleta tija katika  biashara na jamii kwa ujumla hususani kwa wanafunzi wanaofanya masomo ya Kompyuta, sayansi na teknologia ya habari”
“Programu hii imewekwa katika mfumo mzuri ili kuwapa wasichana na wavulana nafasi ya kujiendeleza kuwa wajasiliamali kupitia teknolojia.  Itawasaidia kuwa wabunifu na kujitengenezea ajira kwa kutengeneza program  na bidhaa za kiubunifu zitakazotumika katika jamii zao au mashirika ya umma na kuingiza kipato kikubwa kwa taifa. Kupitia Programu kama ya afriCoderdojo, Science robotics na nyingine nyingi ikiwemo masomo kwa njia ya mtandao yaani E lerning, program za uhandisi, Sanaa na Hisabati, zote hizo ni program zitazotofaidisha jamii na kutoa  suluhisho katika maisha yao ya kila siku”
Dhamira yetu ni kujenga kizazi kipya ambapo katika umri mdogo wataweza kutumia teknolojia ya TEHAMA na kuingia katika elimu ya juu wakiwa tayari na uelewa wa kujihusisha na utengezaji wa programu mbalimbali zitakazoenda sambamba na karne ya sasa na kuleta tija katika kukuza uchumi wa nchi” alisema Mulamula.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad