HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 18 June 2017

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONGOZA HARAMBE YA UJENZI WA KANISA PAROKIA YA ZUZU, DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Kushoto) akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu Pinda walipo mpokea katika makazi yao yaliyopo Zuzu nje Kidogo ya Mjini Dodoma June 17, 2017, kuhudhuria Misa ya kumbukumbu ya Marehemu Mzee Exavery Pinda Baba Mzazi wa Mizengo Pinda, Pamoja na kuongoza Uchangiaji wa Ujenzi wa Nyumba ya Paroko na Ukarabati wa Kanisa la Parokia ya ZUZU.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya familia yake akimkabidhi Mchango wa Shilingi Milioni Kumi, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Paroko pamoja na kufanyia Ukarabati wa Kanisa Parokia ya ZUZU Dodoma. Kushoto ni Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco Msaga . Harambe hiyo imefanyika June 17, 2017 katika Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda yaliyopo ZUZU nje kidogo ya Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu,  Mizengo Pinda akiwaonyesha Wageni waalikwa (hawapo pichani) Shilingi Milioni Kumi Mchango aliokabidhiwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kwa niaba ya Familia yake , Kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Paroko pamoja na kufanyia Ukarabati wa Kanisa Parokia ya Zinje (ZUZU) Dodoma. Kushoto ni Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco Msaga . Harambe hiyo imefanyika June 17, 2017 katika Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda yaliyopo ZUZU Nnje kidogo ya mjini Dodoma. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad