HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 27, 2017

WASHINDI WA LIGI YA CHUO CHA TEKU MBEYA WAPEWA ZAWADI ZAO...

Katika hekaheka za  kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitr Uongozi wa Chuo Kikuu Teofilo Kisanji (TEKU) cha Jijini Mbeya kwa kushirikiana na Serikali ya Wanafunzi TEKUSO na mmoja wa wadau wakubwa wa Vijana Ndugu Amani Kajuna wamefanya bonanza kubwa la michezo kwa kuzishirikisha Timu mbalimbali kutoka ndani ya Chuo na nje ya Chuo ambapo Timu kutoka Mbozi, Uyole, Madereva Bajaji, Madereva Bodaboda zilishiriki kikamilifu kwenye mpira wa miguu, kikapu, pete na mpira wa wavu ambapo washindi walikabidhiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Dkt. Daniel Mosses kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mhe. William Ntinika aliyefungua bonanza hilo na baadaye kuhutubia umati uliokuwepo Chuoni hapo.
Awali, Makamu Mkuu wa Chuo TEKU-Taaluma Dkt. Daniel Gwakisa alisema "Chuo chetu kimekuwa kikijitambulisha kwa Taaluma yake bora na pia kupitia Michezo kwani tunaamini vipaji vya Vijana wetu vinapaswa kuendelezwa ili vikue zaidi", akiongezea Mhadili wa Wanafunzi TEKU Mkufunzi Bi. Stella Seif amesema TEKU wanawalea Vijana (Wanafunzi)  kwa misingi bora kwa kutambua mahusiano ya kada za Cheti, Diploma, Shahada na kada zingine kama za Uzamili.
 Akizungumza na mwanaHabari wetu Rais wa Serikali ya Wanafunzi (TEKUSO) Mhe. Byula Mahona amewaalika wazazi na wanafunzi waliomaliza Elimu za Sekondari na Vyuo kuja kujiunga na Chuo cha TEKU kwani ni Chuo pekee Jijini Mbeya kinachojali na kukuza vipaji vya wanafunzi huku Taaluma itolewayo ni bora, aliongeza kwa kusema moja ya mafanikio ya kukuza vipaji vya wanafunzi ni Chuo kumtoa Miss Mbeya 2016 Eunice John Robert ambaye alishiriki Shindano la Miss Tanzania 2016 na kufanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania Personality 2016, aidha kuna vijana wengine wenye vipaji kama Mzee wa Madodoso, Mpoli Daudi (Wachekeshaji), Goliath, D-nax, G-mafic, Ekka da Music, Peff Mc, Ndaki Black (Wanamuziki) nao wakiwa ni miongoni mwa Vipaji kutokea Chuoni hapo.
Matokeo ya Michezo ya Bonanza yalikuwa kama ifuatavyo: NETBALL:- Teku Queens goli 20 Vs Uyole Queens goli 11 (Mshindi amepata Tshs 50,000/=), BASKETBALL:- Worriers Vikapu 54 Vs Teku Vikapu 50 (Mshindi amepata Tshs 50,000/=), VOLLEYBALL;- Vijana Jiji set 2 Vs Teku set 3 (Mshindi amepata Tshs 50,000/=), Mpira wa miguu kulikua na Timu nne, Bodaboda Fc 2-1 Bajaji Fc,  Unity Fc toka Mbozi 2-1 Home Boys toka Chunya hivyo Fainali ilikuwa kati ya washindi Bodaboda Fc Vs Unity Fc (Dakika 90,Unity Fc 1-1 Bodaboda Fc, mikwaju ya penati Bodaboda Fc 4-5 Unity Fc (Mshindi wa kwanza Tshs 100,000/= wa pili Tshs 50,000/= zilitolewa) 
Mara baada ya mchezo huo kukamilika ndipo mchezo wa Fainali ya Ligi ya Chuo ulichezwa kati ya Timu ya BAED mwaka wa kwanza Vs Timu ya BEDMATHS mwaka wa pili, Matokeo;- BAED 3-2 BEDMATHS (Mshindi wa kwanza amepata Tshs 400,000/= na wa pili Tshs 100,000/=)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad