HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 30 June 2017

WANANCHI WA KIJICHI WAOMBA UKARABATI WA BARABARA YA KIJICHI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jmaii.

Eneo la Barabara  ya Mtoni Kijichi yenye urefu wa Kilo
mita 0.9 ikiwa imeharibiwa na mvua na kusababisha kufungwa kwa barabara hiyo kwa muda wa mwezi mmoja sasa.

Barabara hiyo ni njia kuu ya wapita kwa miguu na magari  hiyo  ni kutokana na njia hiyo kuunganisha maeneo ya Kota za Benki, Nasako, Kota za Polisi na Jeshi  ikiwemo  shule ya Sekondari Neluka na Shule ya Sekondariu ya Mbagala Kuu.

Wananchi wa eneo hilo wamesema kuwa barabara hiyo inahatarisha sana usalama kwani watoto wao wamapokuwa wanapita katika  njia hiyo wanaweza wakajisahau na kutaka kuchungulia ili kuona ndani kuna nini na kuweza kuanguka , pia kuna baadhi ya watoto ambao ni watundu huamua kuingia ndani ya shimo na wengine kushindwa kutoka.

Wameiomba serikali kuikarabati barabara hiyo ambayo inaunganisha maeneo makubwa ya kata ya Kijichi. Picha mbalimbali zikionyesha jinsi barabara ya Mtoni Kijichi inayounganisha maeneo ya Kata ya Kijichi na kusababisha baadhi ya mahitaji muhimu kukosekana kwa takribani mwezi mmoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad