HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 9 June 2017

WADAU WA UCHUMI WAIJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2017/18

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Wadau na wachumi mbalimbali wametoa maoni tofauti kuhusu bajeti ya serikali ya mwaka 2017/2018 iliyowasilishwa jana Bungeni na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango na kusema kuwa ni mapema mno kuisherehekea.

Wakizungumza katika mkutano wa kujadili bajeti hiyo ulioandaliwa na kampuni ya ukaguzi ya Ernst and Young (EY),wamesema, ni vema kusubiri mabadiliko ya sheria ya fedha ili kuja kuona mpango wa utekelezaji wake.
Mkurugenzi wa Utawala na Kodi wa Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), Laurian Justinian akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau na Wachumi mbali mbali wa kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18, ulioandaliwa na Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam Juni 9, 2017.

Wameongeza kuwa, uzoefu unaonyesha kuwa, mara nyingi bajeti inakuwa na mambo mazuri lakini utekelezaji wake unakuwa ni tofauti kwani hata ile iliyopita utekelezaji wake haukuridhisha.
Wamesema kuwa, ni vizuri wananchi wakaacha kusherehekea badala yake kuona utekelezaji na kama ikibidi  waje washerehekee mwezi Juni mwakani.

Akitoa maoni yake katika majadiliano hayo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha  Mzumbe na  Mshauri wa Uchumi, Profesa Honest Ngowi amesema bajeti ya mwaka jana haikutimia kabisa, malengo yalikuwa kukusanya Tirioni 29.5 lakini ilipatikana  Tirioni 20.1 ambayo ni sawa na asilimia 70.1 na bajeti ya mwaka huu ni Tirioni 31.6 ongezeko la tirioni 11. je nini kitafanyika kupata fedha hizo za mwaka huu.

Amesema kuwa kuna masuala mengi ambayo ni lazima yaelezewe sheria ya fedha kwa jinsi itakavyokuwa inatekelezwa ikiwa ni pamoja na kupunguza misamaha isiyokuwa ya lazima.
Amesema bajeti hii inaleta neema kwa wakulima ambao walikuwa wanalipa tozo kwa ukomo wa asilimia tano lakini sasa watakuwa wakilipia ukomo wa asilimia tatu tu.
 Aidha ameongeza pia kuondolewa kwa kodi ya leseni Ya magari kutawapunguzia wananchi mzigo mkubwa, hasa wale ambao magari yao hayakuwa yakitumia klwa muda mrefu lakini bado yalikuwa yanahesabiwa kodo kama kawaida.

Ameongeza kuwa, uchumi wa Tanzania na Africa Mashariki kwa ujumla unaenda kwenye viwanda, na kuna mambo mengi ya kikodi yamejitokeza ya  kulinda viwanda vya ndani kwa maana hiyo kuongezeka kwa kodi kwenye vitu vitakavyokuwa vinaingia ndani yan chi hizo kutakuwa kunalinda soko la ndani.

“Changamoto kubwa itakuwa namna ya kupata fedha zote hizo Tilioni (31.6) hatujajua ni nini cha tofauti kimefanywa tofauti na miaka mingine kusudi kuweza kupata fedha hizo ambazo kwa mwaka jana tulishindwa kupata 29.5 tukaishia kugonga kwenye Trn 20.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na Mshauru wa Maswala ya Fedha na Uchumi, Prof. Honest Ngowi akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau na Wachumi mbali mbali wa kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18, ulioandaliwa na Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam Juni 9, 2017.

Ameongeza kuwa ili kuweza kujaribu kufikia lengo hilo TRA wanatakiwa kukusanya kodi kistaarbu bila ya kutumia nguvu na mabavu, Mkurugenzi wa kodi wa EY Laurian Justinian amesema bajeti inamuelekeo mzuri, inaaanza kuonyesha picha ya kuingia kwenye viwanda but kunamasuala yanatakiwa kuwa na wiano.

Muanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Pangani group Heri Bomani amesema Serikali imekuwa ikiwekeza zaidi kwenye miundombinu na sasa inahama kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Muanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Pangani Group, Heri Bomani akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau na Wachumi mbali mbali wa kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18, ulioandaliwa na Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam Juni 9, 2017. Wengine pichani kutoka kulia ni Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na Mshauru wa Maswala ya Fedha na Uchumi, Prof. Honest Ngowi, Mkufunzi, Mtafiti na Mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dkt. Faisal Issa pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na Kodi wa Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), Laurian Justinian.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad