HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 1 June 2017

MKUU WA MKOA NJOMBE ATEMBELEA MIRADI YA ELIMU NA AFYA

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Christopher Ole Sendeka akiweka jiwe la msingi kwenye  nyumba za waalimu shule ya sekondari ya wasichana Anne Makinda.Nyumba zenye uwezo wa kuishi waalimu 6 katika nyumba moja "6 in 1".
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akikagua uimara wa milango kwenye moja ya madarasa katika shule ya sekondari ya wasichana Anne Makinda.Nyuma yake ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akisisitiza jambo kwa Wananchi (hawapo pichani)  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Luponde mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la OPD  kituo cha afya Luponde wa kwanza kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga
Wananchi wa Kijiji cha Luponde wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa katika mkutano wa hadhara
Mkuu wa Mkoa wa Njombe akiwa katika Picha ya pamoja na uongozi wa wanafunzi shule ya sekondari ya wasichana Anne Makinda,Shule hiyo ya Kata ilifanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana na kushika nafasi ya Tano Kimkoa na Nafasi ya Kwanza Kiwilaya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad