HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 9 June 2017

MANISPAA YA UBUNGO YASAINI MIKATABA 30 YA UKANDARASI

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam imetiliana saini ya mikataba 30 yenye thamani ya Sh. bilioni nne na Wakandarasi kutekeleza shughuli mbalimbali katika halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa utilianaji saini hizo uliofanyika katika Ofisi za Halmashauri hiyo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo alizitaja shughuli zitakazohusika katika mikataba hiyo kuwa ni pamoja na usafi, barabara  na miradi ya maji.
 “Manispaa yetu ina miezi minane tu lakini tumefanikiwa kusaini mkataba 30 ya miradi mbalimbali, tunaposaini mikataba hii inaonesha wazi kuwa Manispaa yetu inakua.
“Ombi langu kwenu, nendeni mkatekeleze kile kilichopo kwenye mikataba na bahati nzuri siwafahamu sitaweza kusita kuchukua hatua kama Meya, nitasimamia sheria sitapindisha pale nitakapoona kazi imeenda ovyo sitakuwa tayari kufungwa pingu” amesema Kayombo.
Kayombo aliwataka wakandarasi hao kuhakikisha wanatekeleza miradi waliokubalia isiishie kusaini kisha wakapotelea mitini.
Naye  Meya wa Manispaa hiyo, Boniphace Jacob, aliwataka wakandarasi hao kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo katika kiwango walichokubaliana na kuwa atakayetekeleza kinyume atanyang’anywa na kupewa mtu mwingine fedha zitarudishwa .
“Ukipewa miezi miwili ikiisha kabidhi mradi, mkurugenzi ukikuta mtu anayefanya kazi ya usafi hajasafisha au  mtu yeyote atakayekiuka mkataba tusiwe na aibu ya kumwajibisha” amesema Jacob.
 Meya wa Ubungo,  Boniface Jacob (kushoto)  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kusaini mikataba 30 yenye thamani ya Sh.bilioni Nne na wakandarasi kutekeleza shughuli mbalimbali katika Halmashauri hiyo. kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo,
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo akizungumza katika hafla ya kusani mikataba 30 yenye thamani ya Sh bilioni nne na wakandarasi kutekeleza shughuli mbalimbali katika halmashauri hiyo.
 Meya wa Ubungo, Boniface Jacob (katikati)na  Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo (wa kwanza kulia ) wakisani mkatamba na Mkurungenzi wa Kampuni ya Invostment , Rukia Punzi leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo akibadilishana hati za makubalino na Mkurungenzi wa Kampuni ya Invostment Rukia Punzi leo jijini Dar es Salaam.,katikati ni Meya wa Ubungo Mh. Boniface Jacob.
Watendaji wa Manispaa hiyo kiwakatika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad