HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 2, 2017

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI (TAA) YAADHIMISHA SIKU YAMAZINGIRA DUNIANI KWAKUFANYA USAFI

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) imeshiriki kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku mazingira duniani.

Wafanyakazi wa mamlaka hiyo wameshiriki shughuli hizo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, ambayo kitaifa inaadhimishwa kesho katika Wilaya ya Butiama, mkoani Mara.

Akizungumza leo wakati wa kufanya usafi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Salim Msangi amesema, ndege za abiria zimekuwa zikizalisha hewa ya ukaa kwa asilimia mbili duniani kote, hivyo ni muhimu kupanda miti maeneo ya viwanja vya ndege ili kutunza mazingira.

Amesema kila mwaka wamekuwa wakipanda miti katika maeneo ya viwanja vya ndege ili kufyonza hewa ya ukaa ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia kuharibu mazingira na kuongeza joto.

"Lakini pia nimeagiza mameneja wote kuhakikisha wanapanda na nitakuwa natoa zawadi kila mwaka kwa meneja atakayeonekana kufanya vizuri," amesema Msangi.

Amesema utunzaji wa mazingira ni muhimu kwani binadamu wote na viumbe hai vingine vinahitaji mazingira na kwamba hata kaulimbiu ya kitaifa ya mwaka huu ya “Hifadhi mazingira, Muhimu kwa Tanzania ya Viwanda” haiwezekani kuwa na viwanda katika mazingira ambayo si salama.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Salim Msangi wa (kwanza kushoto) akiongoza ufanyaji  katika maeneo yanayozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa Mamlaka Viwanja vya Ndege nchini (TAA), wakiendelea na  usafi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka Viwanja vya Ndege nchini (TAA),Salim Msangi akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad