Meneja wa tigo mkoa Tabora Brighton akitoa neno la kuwakaribisha wageni kwa niaba ya Meneja wa tigo mkoa Kigoma wakati wa hafla ya futari ya pamoja baina ya watoto wanaoishi kwenye kituo hicho na uongozi wa tigo ambayo ilienda sambamba na kukabidhi misaada ya vyakula mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 1.2.
Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga ( wa pili kulia) na Mkurugenzi wa kanda ya ziwa wa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo Gwamaka Mwakilembe (kulia) wakikabidhi kwa uongozi wa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha MWOCACHI misaada mbalimbali vya vyakula kwa ajili ya kituo hicho misaada ambayo ilienda sambamba na futari ya pamoja baina ya viongozi wa tigo,wadau mbalimbali na watoto hao iliyoongozwa na Mkuu wa wilaya Kigoma.
Wageni waalikwa na watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima na mazingira magumu cha MWOCACHI cha mjini Kigoma wakishiriki kwenye futari ya pamoja iliyoandaliwa na kampuni ya simu ya mkononi ya tigo kwa watoto hao.

No comments:
Post a Comment