HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 16, 2017

CRDB YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUWAPATIA ZAWADI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya CRDB imeadhimisha siku ya  Mtoto wa Afrika kwa kuwapatia zawadi watoto mbalimbali ambao wazazi wao waliwafungulia akaunti za Junior Jumbo huku wakiwa wamewekewa fedha mara kwa mara.

Akitoa zawadi hizo, Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe  Nomina Msoka amesema kuwa watoto hao waliopatiwa zawadi ni kutokana na wazazi wao kuwawekea fedha mara kwa mara na hata akiba za akaunti zao zina kiasi kikubwa cha fedha.

Nomina amesema kuwa, wazazi wanatakiwa kuwafungulia na kuwawekea watoto wao fedha mara kwa mara iili kuwandaa na maisha ya baadae ikiwemo katika kulipia ada za masomo yao na pia upo taratibu wa wazazi kuwaekea hela kupitia akaunti zao..

Amesema mbali na hilo, CRDB wameweza kuandaa michezo mbalimbali ya watoto kwa ajili ya kujumuika pamoja na wenzao na kufahamiana zaidi.
Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe  Nomina Msoka akiwa amembeba mtoto Kinora Brown na kumkabidhi zawadi yake ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  kwa mama yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka. 
 Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  mtoto Orley Mwanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
 Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  mtoto Tonia Naivasha  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  mtoto Rashidi Jumbe wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka  akiwa katika picha ya pamoja na watoto aliowakabidhi zawadi za mebegi ya Junior Jumbo Akaunti  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.

  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka   akizungumza na watoto hao baada ya kumalizika kwa zoezi la ugawaji zawadi  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
Watoto waliojitokeza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika wakiwa wanacheza michezo mbalimbali iliyoandaliwa na tawi la benki ya CRDB Azikiwe. Picha zote na Zainab Nyamka.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad