HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 2, 2017

BARAZA LA WAGANGA WAIOMBA WIZARA YA AFYA KUWAPA ELIMU YA UGONJWA WA EBOLA.


Katibu Mkuu wa Baraza la Waganga Shaka Mohamedi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na serikali kutoa elimu ya ugonwa wa Ebola na dalili zake kwa waganga wa Tiba asilia leo Jijini Dar  es salaam.

Na Ashraf Said.

Baraza la Waganga laiomba serikali kutoa mafunzo maalum kwa waganga wa tiba asilia kuwapa elimu na kuufahamu ugonjwa wa Ebola na dalili zake ili kuweza kushiriki katika kutoa taarifa pindi watakapokutana na mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa huo

Mapema wiki hii Wizara ya Afya,maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto kupitia kwa Waziri Ummy Mwalimu walitoa taarifa rasmi zinazohusu ugonjwa wa Ebola na kusema kuwa bado haujaingia nchini na watanzania wasiwe na hofu kwani serikali iko makini katika kuhakikisha wanapambana nao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza la Waganga Shaka Mohamedi ameiomba Wizara ya Afya,maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto kuangazia zaidi kwenye utoaji wa elimu dhidi ya ugonjwa wa Ebola kwa waganga wa tiba asilia ikizingatia na wao ni moja ya watoaji huduma za kiafya kwa jamii inayowazunguka.

Shaka amesema waganga wa tiba asilia watakapofahamu dalili za ugonjwa wa Ebola itakuwa ni rahisi sana kuweza kutoa taarifa kwa Serikali kulingana na huduma wazitoazo na ukaribu uliopo baina yao na jamii

"Naipongeza wizara ya Afya kwa kuchukua hatua za haraka na mapema ikiwa ni tahadhari za kuzuia ugonjwa wa Ebola kuingia nchini kutoka nchi jirani ya Congo DRC,lakini pia naomba wizara hii kuchukua hatua za ziada kuhakikisha wananchi kuwa na uelewa mpana wa dalili za ugonjwa wa Ebola,'' Amesema.

Licha ya hayo,katibu mkuu wa baraza la waganga BAWATA ameonya vikali waganga wote wanaohudumia au kujinadi kutoa tiba asilia kwa jamii hali ya kuwa hawatambuliki kwenye Baraza hilo,ni kosa kisheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad