HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 17, 2017

YANGA YAMWAGIWA MABILIONI YA UDHAMINI NA SPORTPESA LEO.



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya Nchini Kenya SportPesa imeimgia mkataba na klabu ya Yanga wa udhamini wa miaka mitano ukiwa na thamani ya takribani bilioni 5.

Uwekaji huo wa saini umefanyika leo katika makao makuu ya Klabu ya Yanga ukishuhudiwa na wanachama mbalimbali wakiongozwa na viongozi wa Kamati ya Utendaji akiwemo Makamu Mwenyekiti Clement Sanga.

Akizungumza baada ya kutia saini hati ya makubaliano ya mkataba huo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Sanga amesema kuwa mkataba huu utakuwa na faida kubwa sana kwa klabu kwani wameweza kuongelea mambo mbalimbali ya kimaendeleo yakiwemo soka la Vijana.

Sanga amesema ni mara ya kwanza katika mikataba waliyowahi kuingia akiwa kama kiongozi umekuwa na viyi vingi sana vya kimaendeleo ukiachilia fedha wanazozipata za udhamini.

"katika mikataba tuliyowahi kuingia nikiwa kiongozi wa Yanga huu ni moja ya mkataba tuliozungumzia maendeleo ya klabu mbali na fedha tunazozipata ila tumeangalia katika Uwanja wetu wa Kaunda na hata soka la Vijana na mambo mengine mengi,"amesema Sanga.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa SportPesa nchini Tanzania Tarimba Abbas amesema Yanga watapata zaidi ya bilion 5 kwa miaka mitano na kwa mwaka wa kwanza wataanza kwa kupata milion 950 na itaongezeka kwa asilimia 5 kila mwaka na hii inakuwa klabu ya pili kuweza kuingia nao mkataba baada ya Simba kusaini wiki iliyopita.

Tarimba amesema makubaliano yao na Yanga yapo ambayo hayajawekwa wazi ni ya ndani ya klabu na si vizuri kuyasema ila kuhusu bonus zitakuwa sawa ambapo timu ikichukua ubingwa wa ligi au kagame au michuano yoyote ya kimataifa kutakuwa na fedha watakazopatiwa nje ya fedha ya udhamini.

Klabu Yanga inatarajiwa kufaidika na udhamini hasa kwa makubaliano waliyoingia ya kukarabatiwa uwanja wa mazoezi, kukuza vipaji vya soka la vijana pamoja na kupatiwa gari la wachezaji.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov akikabidhiana hati ya makubaliano ya mkataba na Mkamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga ukiwa ni mkataba wa miaka kitano wenye thamani ya zaidi bilioni 5, uwekaji huo wa saini na makabidhiano yamefanyika leo Makao Makuu ya klabu hiyo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa SportPesa nchini Tanzania Tarimba Abbas na kushoto ni Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Charles Mkwasa.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya mkataba wa udhamini baina ya Klabu ya Yanga na Kampuni ya Michezo ya kubahatisha ya SportPesa ya nchini Kenya, uwekaji huo umefanyika leo Makao Makuu ya klabu hiyo Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad