HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 20, 2017

YANGA WAKABIDHIWA KOMBE LAO MWANZA, MBAO YANUSURIKA KUSHUKA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Ligi Kuu Tanzania Bara imemalizika leo kwa timu ya Yanga kutawazwa ubingwa wa msimu wa 2016/17 ikiwa ni  mara 27 toka ligi kuanzishwa.

Yanga waliokuwa ugenini dhidi ya Mbao iliweza kupoteza mechi hiyo ya mwisho lakini walitawazwa ubingwa kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa dhidi ya Mahasimu wao wakubwa Simba.

Katika mechi hiyo iliyoanza sa  10 Mbao waliandika goli lao la kwanza na la ushindi katika kipindi cha kwanza  ambapo liliweza kudumu mpaka dakika 90 kumalizika.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Ludovic Charles kutoka Tabora ilikuwa ya kukamiana kwa kila upande huku akionekana kushindwa kuuhimili mchezo huo.

Baada ya kumalizika kwa mechi nane za Ligi zilizochezwa kwa mda mmoja timu ya Toto Afrika ya Mwanza na African Lyon zimeshuka daraja zikiungana na JKT Ruvu iliyokuwa tayari imeshajikatia tiketi ya kurudi daraja la kwanza.
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Wakiwa wanashangilia baada ya kutawazwa mabingwa leo Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya tatu mfululilzo.
 wachezaji nwa Yanga wakipokea medali zao za ubingwa baada ya kutawazwa mabingwa kwa mara ya 27 na mara ya tatu mfululizo.
Kikosi cha Mbao kilichocheza dhidi ya Yanga leo katika Uwanja wa CCM Kirumba na kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
            Kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Mbaoleo katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Mwali kabla ya kukabidhiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad