HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 16, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA MILIONI 12 MCHANGO WA SERENGETI BOYS


Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea jumla ya shilingi 12,000,000 kutoka kwa Kampuni ya Multi Choice, 
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa ajili ya kuisaidia timu ya Serengeti Boys.

Dkt. Mwakyembe amezipokea fedha hizo leo Jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari na kuahidi kutoa taarifa ya kiasi cha fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali mwishoni mwa mwezi huu.

“Nawashukuru wadau wote wanaoendelea kuichangia timu yetu ya Serengeti Boys, leo nimepokea shilingi 10,000,000 kutoka Kampuni ya Mult Choice, shilingi 1,000,000 kutoka MISA TAN pamoja na shilingi 1,000,000 kutoka TAKUKURU”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Ameongeza kuwa timu imeanza mashindano hayo vizuri japokuwa wametoka bila kufungana na timu ya Taifa ya Mali ambayo ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo.

Aidha, ameahidi kuwa mchezo dhidi ya Timu ya Serengeti Boys na Timu ya Angola itakayochezwa Mei 18 mwaka huu itarushwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa (TBC).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa MISA TAN, Salome Kitomari amesema kuwa waandishi wa habari wameamua kuisaidia timu hiyo sio kwa kutumia kalamu zao kuwatangaza katika vyombo vya habari tu bali imeamua kuwasaidia kwa kuwachangia fedha.

“Tumeamua kuichangia timu yetu ili tuwape moyo zaidi wa kufanya vizuri kwani wameonesha jitihada katika mchezo wa mpira wa miguu,” alisema Bi. Salome. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad