HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 14 May 2017

WANAFUNZI WA CHUO CHA STELLA MARIS MTWARA WAPIGWA MSASA JUU YA UMUHIMU WA EAC

Mabalozi wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo Mayenga pamoja na Suzane William Mollel wamekutana na Wafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara, kwa lengo la kutoa mafunzo na kuwahamasisha Wanafunzi wa vyuo vikuu (Vijana) nchini kote, kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuuimarisha katika Mchakato wa Jumuiya hiyo Kikanda, katika Warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo, Mei 12, 2017. Jumla ya Wanafunzi 230 walihudhulia Warsha hiyo.
Mabalozi wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo Mayenga pamoja na Suzane William Mollel (wa tatu na nne kushoto) wakiwa wameshika Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya Wafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara, wakati wa Warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo, Mei 12, 2017.
Naibu Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel (aliyesimama) akiwasilisha mada katika Warsha ya siku moja kwa Wafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara, juu ya umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuuimarisha Mchakato wa Jumuiya hiyo Kikanda, iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo, Mei 12, 2017. 
 Wanafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara, wakimsikiliza kwa makini Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo Mayenga.
Sehemu ya wanafunzi hao wakiwa kwenye Warsha hiyo.
Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo Mayenga akikabidhi Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara akikabidhi Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad