HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 13, 2017

VIDEO: TRA YAKANA KUMKADIRIA KODI YA SHILINGI MILIONI 400 MSANII DIAMMOND

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said .

MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nassib Abdul ( Diamond Platnamuz) kulipa kodi ya shilingi Milioni 400. 

Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam. 

“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza .

“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo. 

“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. Awali akifungua semina hiyo. Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi. 

“Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo. 

Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chombo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za serikali kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma. 

“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Mei 13, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi. Angella Msangi na kushoto ni Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Mwangosi 
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (kulia), akiwakaribisha waandishi wa habari kwenye semina. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina, Bi. Angella Msangi .
Mkutano huo ukiendelea
Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad