HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 12 May 2017

UZINDUZI WA LIGI YA MABENKI "BRAZUKA KIBENKI" WAFANYIKA, TIMU 16 KUSHIRIKI MWAKA HUU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


UZINDUZI wa ligi ya mabenki umefanyika huku timu zikiongezeka na kufikia 16 kushiriki katika mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete (netball) huku droo ya makundi ikifanywa.

Ligi hiyo inayotambulika kama 'Brazuka Kibenki' inatarajiwa kuanza Julai Mosi mwaka huu zikiwashirikisha timu 16 kutoka mabenki tofauti nchini huku mwaka huu kukiwa na ingizo jipya ya benki ya UBA.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo ya Mabenki mratibu Raymond Bunyinyiga amesema kuwa huu ni mwaka wa tatu toka waanze kuwa na ligi ya mabenki ila mwaka huu ushindani utakuwa mkubwa zaidi kwani kila timu imeonekana kujipanga kuchukua ubingwa mwaka huu.

Raymond amesema kwa mwaka huu timu zimeongezeka mpaka kufika 16 kwani mwaka jana zilikuwa timu 14 pamoja kila timu kupewa sheria 17 zinazoendesha shindano hilo ambapo ziliweza kupitishwa waandaji wa ligi hiyo kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).

"Tumeweza kufikisha timu 16 mwaka huu kukiwa na maingizo mapya ya mabenki pia kila timu inatakiwa kufuata sheria zilizowekwa ili kuepuka kuondolewa katika ligi hiyo kwa kutokufuata sheria ikiwemo ya kuwachezesha wachezaji ambao ni mamluki na iwapo utatambulika umefanya hivyo utaondolewa moja kwa moja pamoja na kulipa faini,"amesema Raymond.

Mbali na hilo pia ameishukuru Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa jitihada kubwa wanazozionesha katika kuinua michezo ikiwemo na kushirikiana na kuwapa ushauri katika kuandaa ligi hiyo ya Brazuka Kibenki.

Ligi hiyo itakayoanza Julai Mosi itafanyija katika Viwanja vya Gymkhana na inatarajiwa kuwa katika hatua ya makundi 4 kwa kila kundi kuwa na timu 4 na zitachezwa kila Jumamosi kwa kipindi cha miezi minne na zawadi ya Mshindi wa kwanza itakuwa ni kombe huku kukiwa na zawadi zingine zaidi ya mia moja kwa washiriki ambao ni mabenki pamoja na wachezaji na ada ya kuingia ni kiasi cha Shilingi milion moja na laki mbili kwa kila timu (1,200,000).

 Mratibu wa Ligi ya Mabenki Raymond Bunyinyiga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo inayojulikana na Brazula Kibenki inayotarajiwa kuanza Julai Mosi mwaka huu na timu 16 kutoka mabenki tofauti kushirki katika michezo ya soka na netboli.Kushoto ni Nahodha wa timu ya DTB  Iddy Yakoub.
 Mratibu wa Ligi ya Mabenki Raymond Bunyinyiga akionyesha timu shiriki zitakazoumana kwne ye ligi ya Mabenki Brazuka Kibenki Julai Mosi mwaka huu.
Wawalishi wa mabenki wakiwa wanaonyesha vikatarasi vya makundi walivyokuwa wamechagua jana katika Uzinduzi wa ligi ya Mabenki Brazuka Kibenki itakayoanza Julai Mosi mwaka huu.

Waandishi wa habari wakiwa wanafuatilia uzinduzi huo uliofanyika jana.

Picha na Zainab Nyamka.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad