WANAKIKUNDI cha upakasaji mikoba, makawa, vipochi vya ukili na upandaji miti cha ‘Subira njema’ kilichopo kijiji cha Changaweni Wilaya ya Mkoani Pemba, ambao wengi wao ni watu wenye ulemavu, wakiwa kazini katika kazi yao hiyo ambapo mkoba mmoja wa kisasa wenye zipu ni shilingi 20,000 hadi shilingi 25,000, (picha na Haji Nassor, Pemba)
WAJASIRIAMALI kisiwani
Pemba, wakiwa na sabuni za michi, nje ya ukumbi wa kiwanda cha mafuta ya
Makonyo Wawi Chakechake baada ya kuhitimu mafunzo hayo, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
NA HAJI
NASSOR, PEMBA
“………kozi
mwana mandanda kulala na njaa kupenda…………..”
Huu ni msemo maarufu ambao unatumika
katika visiwa vya Unguja na Pemba na hata kuleTanzania bara kwa baadhi ya
maeneo.
Hapo zamani za kale, wazee wetu
walikuwa wanapenda zaidi kutumia misemo kuliko bakora, kwa lengo la
kuwafundisha na kuwaasa wanaowalea
‘’Maskini enzi zetu zimeshapita ‘’baadhi
ya wazee wenye umri wamekuwa wakisema kwa karne hii.
Katika zama hizi za Sayansi na
Teknologia, si wengi ambao wanajua maana ya misemo kadhaa, bali wengi
wanaisikia tu na kutokua na jawabu rasmi.
Kwa hapo zamani misemo ni miongoni mwa
bakora inayoweza kutumika kupiga mtu na mwenye akili timamu.
Ilikuwa kwa hapo karne hiyo, misemo, inaweza
kujua kwamba muda gani mtu anatakiwa afanye nini, au ache kufanya jambo fulani,
na kuwepo kwa matunda.
‘Ama kweli lishalo vuusha sidau’’,
ndio maana leo hii waliowengi hawathamini na wala hawajali misemo mbali mbali
ya wazazi wetu ambao ndio waliotuzaa.
Nisiende mbali naogopa nisije
nikageuka muazima jamvi…….. kwa wale wanaofahamu ni kwamba mara husau lengo
alilokwendea kwa jirani.
Nami hapa naogopa na naheshimu nisije
nikalisahau lengo langu ndani ya waraka huu wa makala ambayo kwa hakika
imenivutia na ndio maana nikaamua kuiandika.
Lengo hasa ni kikundi cha ushirika cha
wanawake tena wenye ulemavu kilichopo kijiji cha Changaweni wilaya ya Mkoani
ndani ya Kisiwa cha marashi ya karafuu.
“Ile kauli isemayo………. wanawake
wanaweza hapa haikwenda kombo kwa wanawake hawa ukizingatia wao ni wenye ulemavu”,
ni kweli kabisa wanaweza.
Si wengine bali ni wanaushirika wa” Subira
njema” wanawake ambao ni walemavu na hapa nilitaka kujua historia ya
wanaushirika hawa.
Nilianza kuweka kalamu na shati langu
sawa, wakati nikizungumza na Amina Abdalla Said, yeye ndie Mwenyekiti wa
wanaushirika hao.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo,
ushirika wao ambao wanajituma usiku na mchana kwa lengo lakupata riziki zao za
halali, unajishughulisha na kazi mbali mbali.
‘’Sisi hapa twapakasa mikoba ya ukili
lakini hii ya kisasa, nikamuliza hata mikoba ya ukili kuna ya kisasa kumbe?
akajibu ndioo huku akicheka.
Ushirika huo wa wanawake wenye ulemavu
ulianza mwaka 2009, ukiwa na wanachama 10 wakiwemo wanaume wawili.
Kwa sasa unajishughulisha zaidi na utengenezaji
wa sabuni za kufulia, kuoshea vyombo na kuogea na vipochi vya ukili.
Mwenyekiti akizungumza na mwandishi wa
makala haya, hapo Changaweni Mkoani, hakuacha kuniambia kuwa wanatengeneza
sabuni, je wanayo mashine.
Suali hili nilimtupia tena Mwenyekiti
huyo na bila ya kusita, akasema kuwa ‘tunatumia mikono na ndoo na hatuvai hata ‘glavu’
yaani kukinga ngozi’’,alisema.
Hili linatokana na kutokuwa na vifaa vya
kutengenezea sabuni na kukumba na kemikali kadhaa ikiwa ni pamoja na ile ya ‘kastik’
ambayo huichanganya na malighafi nyengine.
Salama Mwadini Juma ambae ni
mwanachama wa ushirika huo wa ‘’Subira njema‘’ anasema hili hasa la kukosa mashine,
limekuwa likiwahatarishia usalama wa afya zao.
Anaona kuwa, licha uzalishaji huo kuwa
ni muda mrefu, lakini hadi sasa hawajapatiwa mashine na kuendelea kuzalisha
sabuni kwa kutumia mikono.
Akizungumzia suala la soko la bidhaa hiyo
Mshika fedha wa ushirika Nassra Yussuf Khalifan, bado halijanyanyuka vyema, na
wamekuwa wakiuza kwa kubahatisha.
‘’Kwa sasa wateja wetu ni hawa
wanaokuja hapa hapa na kujinunulia, lakini lile soko kubwa halipo, lakini pia
kwa sababu bidhaa haziko kwenye kiwango’’,alisema.
Ushirika huo kwa sasa hauna ‘pekingi’
ya biashara zao, jambo ambalo huwenda ikawa ni sababu moja wapo ya kutokuwa na
soko la hali ya juu.
Miongoni mwa aina sabuni
wanazotengeneza kwa kutumia malighafi za mchachai, mkaratusi, na nyengine baada
ya kupewa mafunzo kupitia Umoja wa watu wenye Ulemavu Zanzibar UWZ.
Ushirika huu, kwa muda wa miaka nane
sasa wanaendelea kuweka maisha yao rehani, kwa kuendelea kutumia mkono yao
kutengeneza sabuni kw aukosefu wa mashine.
Soko la uhakika hasa la bidhaa ya
sabubu ndani ya ushirika huu, bado ni kizungumkuti, maana hulazimika
kuzikopesha ili zisijewaharibikia mikononi mwao.
Sabuni zenye thamani ya shilingi
150,000 sawa na michi 50 ya sabuni ziko mikononi mwa wateja wao, maana hawana
soko la uhakika na vyenginevyo wakiogoa kuzikopesha ndio hawafikii malengo.
Hivi karibuni kwa kutumia mikono yao,
walizalisha sabuni boksi tano na kila moja, huingiza michi 25, ambapo boksi
tano zenye michi 75 sawa na shilingi 225,000 walibahatika kuziuza.
Mbali na mambo hayo ya usafi na povu, lakini
ushirika huu ulionzishwa mika nane iliopita, unajishughulisha na utengenezaji
wa mikoba ya kisasa na vipochi vya ukili ,mikeka na makawa .
Kwenye ushirika huu wanauza mkoba
mmoja kwa bei ya shilingi 10,000 hadi shilingi 15,000 kutokana na ukubwa wa
mkoba huiska.
‘Lakini pia ipo mikoba mengine hii
ambayo sio ya kileo sana hii tunauza kati ya shilingi 8,000 hadi shilingi 7,000
alisema huku akiwa na mkoba mkononi Nassra Yussuf.
Kwa kwenye ushirika huo, pia kwa vile
wajishughulisha na upakasaji wa makawa, huwezi kulipata kama huna shilingi shilingi
3,500 au shilingi 4,000.
Ukija kwenye zulia la usumba ambapo
ushirika huu unatengeneza na kuliuza kati ya shilingi 7,000 kwa moja, wakati
mkeka mmoja ni wenye ukubwa ni shilling.40,000.
Ushirika huo wa wanawake baada ya
kuhangaika huku na kule, kwa sasa umeshaweka mikono yake wazi kwenye benki ya
Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kuwa na ‘Account’ namba 041207000765.
Kwa mujubu wa mshikafedha wa ‘Subira
njema’ Nassra anabainisha pia kibakuli chao hicho hakiko kitupa maana kina
akiba ya zaidi ya shilingi laki tano (500,000).
Toka kuanza ushirika huo hadi sasa, hawajawahi
kupata msaada wowote kutoka Serekalini, ingawa wameshaomba mara kadhaa.
Jambo hilo linawashangaaza sana maana
walitakiwa kuanzisha vikundi vya aina hiyo, lakini kwa sasa mambo ni magumu,
kwao kutokana na kuwa hawakumbukwi.
‘’Maisha ni safari refu na safari ni hatua ‘’,
na hatua lazima unyanyue mguu lakini sisi mguu wetu umekwama na tunahitaji kukwamuliwa’’,
alifafanua Mshikafedha huyo.
Sikutosheka na hayo nilitaka kujua
changamoto ambazo zimewakabili, ili kuweza kujua jinsi ya kuwasaidia kupitia
ukurasua huu.
Salama Mwadini Juma ambae ni mjumbe katika
ushirika huo wa wanawake wenye ulemavu hakunyamaza kimya, akasubiri kila kitu
kusemewa alinyanyua mdomo tena kwa sauti akiwa na tamaa kubwa ya kupata msaada.
Bi Salama anasema kuna changamoto
mbali mbali ambazo zimewakabili katika ushirika wao, ikiwa ni pamoja na ukosefu
wa vitendea kazi.
‘’Ofisi hatuna, sabuni mapaka leo
twafanyia mikono, soko madhubuti ambapo haya yanatukwaza sana’’,alieleza huku
akiwa na masikitiko.
Asya Ali Hamadi, ambaye nae ni mjumbe katika
ushirika wa ‘’Subira njema‘’ suala la kufanyia sabuni ndani ya nyumba ya
mwanachama ni hatari hata kiusalama wa watoto wao.
Aliomba Serekali kupitia Wizara ya
Uwezeshaji kuwaangalia kwa jicho la huruma, kwani wakiwapatia msaada wataweza
kujiendeleza zaidi.
Lakini aliwageukia wanawake wenzake
wale ambao hawajishughulishi na chochote, wajitume na waondokane na dhana ya kuwa
mwanamke siku zote ni mtu wa kukaa ndani.
Akasema hiyo ni dhana potofu, na
anaetaka kujua juu ya hilo afike ‘Subira njema’ Changaweni, kwani wanawake
wanaweza hata kama hawakuwezeshwa.
Ndio hapa pakuanzia kwa Wizara yetu ya
uwezeshaji, kwani kwa muda mrefu wanawake walionekana hawawezi ndio maana
wakabakia majumbani na kuhudumia watoto.
Asha Hassan Makame, ambae hajajiingiza
kwenye kikundi chochote cha ushirika, anasema natamani sana ingawa, changamoto
anayoiona ni kutengwa kwa kukoseshwa vifaa.
“Vipo vikundi vingi vya wanawake,
lakini huona kama vile maisha yao hayajabadilika yako sawa na yangu, sasa
Napata wasiwasi wa kujiunga na mimi’’,anasema.
Ingawa Maulid Saleh Hamad wa Kiuyu
yeye anasema kama yupo mwanamke Tanzania hii hajajiunga na wala hanadhamira ya
kujiingiza kwenye ushirika amechelewa.
Mratibu wa TAMWA Zanzibar Mzuri Issa,
yeye anaona ili uwanaharakati wa mwanamke utimie ni kukusanya nguvu zao pamoja.
“Baada ya lazima sasa serikali ione
umuhimu wa kuwasaidia vifaa kama hao wanawake wenzetu wa Changaweni, ili
wasonge mbele’’,alifafanua.
Mlekwa Makame Hija wa Mkoani, anasema
kama wanawake wakishajiunga pamoja na kusaidiwa vifaa, wanaweza kupiga hatua
moja kubwa ya kimaendeleo.
Ingawa sheikh Nassor Khamis wa
Mizingani anasema lazima wanawake waliopata ruhusa kwa waume zao, kujiingiza
kwenye vikundi hivyo, wasisahau wajibu na majukumu yao, kama walivyo kwa
wanaume.
Mkuu Wa mkoa wa kusini Pemba,
Mwanajuma Majid Abdalla anasema jambo la kwanza ni mwanamke kukubali kujiingiza
kwenye njia za kujikomboa.
“Unajua serikali na hata wafadhili
hupenda zaidi kuwasiaidia wanawake waliojikusanya, sasa lazima tuhamasishahe
kuefanya hivi, ili tujikomboe’’,anashauri.
Naibu Katibu mkuu wozara
inayoshughulikia wanawake na watoto Mauwa Makame Rajab ameutaka uongozi wa
ushirika huo, wasisite kufika wizarani ili kupata ufumbuzi.
“Waende wizarani baada ya kujua
gharama ya mashine ya kutengeneza sabuni, kisha wanaweza kupewa maelekezo ya
kuandika barua na kuomba mkopo’’,anashauri.
Anesema haipendezi na ni hatari
kushika kemikali kwa mikono wakati wanajikomboa kwa kutengeneza, sabuni waombe
mkopo wanunue mashine.
Shemsa Hakim Khamis ambae amejiari
kwenye gari ya TAX eneo la uwanja wa ndege Pemba, anasema lazima wanawake sasa
wawe na njia ya kujikomboa.
“Maisha sasa yapaa, lazima kila mmoja
ndani ya familia awe chanzo cha mapato, ili kuimarisha ndoa na
familia’’,alishauri
Kwa upande wake mjasiriamali anaejishughulisha
na ususi wa mikoba ya kisasa, wa Kiuyu wilaya ya Wete Nassra Salim Mohamed
anasema hata kama mwanamke ameolewa, lakini kujiingiza kwenye uwanaharakati ni
lazima.
Asha Muhidin Mjaka wa Wawi ambae
hajajiingiza kwenye ujasiriamali, anasema bado hajapata elimu ya juu ya jambo
hilo.
“Mimi sijapa elimu na ndio maana hadi
sasa naendelea na kilimo cha migomba, mihogo na mpunga peke yangu’’,alisema.
Mwakilishi wa jumuia ya watu wenye
ulemavu Zanzibar UWZ Pemba Salum Abdallah, amekitaka kikundi hicho cha ususi wa
mikoba kuwashirikisha ili kuwatafutia mashine.
“UWZ ipo kwa ajili ya kuwahudumia
wanachama wake, sasa wanapokwama waje ili tuone wanaendeleza njia yao ya
kujikomboa’’,alishauri.
Daktari Makame Hassan Makame, anasema
kemikali na mchanganyiko wa dawa nyengine zikiingia kwenye ngozi ya mwanadamu
husababisha madhara kadhaa.
“Moja ni ngozi kukosa hisia unaweza
kuungua moto ukachelewa kufahamu, lakini pia ngozi kukosa kuhifadhi
mafuta’’,alisema.
No comments:
Post a Comment