HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 14, 2017

TCRA yawatahadharisha watumiaji wa kompyuta juu ya shambulio la Kirusi Kiitwacho WANNACRY kwenye kompyuta

Shambulizi la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani.

Kampuni ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000 za programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama 'WannaCry' duniani.

Kuna ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi.
Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na Uskochi.

Programu hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola 300 ili kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta.Siku nzima, mataifa ya Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.

Hii ni Tahadhari Iliyotolewa  na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA  kuhusu Kirusi hicho

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad