HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 31, 2017

TAIFA STARS KUANZA MAZOEZI USIKU NCHINI MISRI KUJIANDAA NA LESOTHO

Alfred Lucas, Misri.
TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inatarajia kuanza mazoezi jioni ya leo  kujiandaa na mchezo wa kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.

Stars walioingia majira ya saa 7 usiku na kufikia katika mji wa Alexandria, Misri uliweza kuwasili salama na kwa niaba ya timu nzima, Kocha Mkuu, Salum Shabani Mayanga pamoja na viongozi wengine akiwamo Mkuu wa Msafara, Wilfred Kidao walishukuru Mungu kwa kusafiri salama hadi kufika hapa Alexandria kwa ajili ya kambi ya wiki moja kujindaa kucheza na Lesotho.

Akizungumza mara baada ya kukagua viwanja vya mazoezi leo asubuhi, Kocha Mayanga amesema  “Programu ya mazoezi kwa timu hii itaanza leo saa 2.00 usiku ingawa siku nyingine nitafanya asubuhi na jioni.”

Taifa Stars inayopiga kambi nchini Misri, inajiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam mchezo uliopangwa  kuanza saa 2.00 usiku.

Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ wakiwa na timu za Uganda na Cape Verde kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Kocha Salum Mayanga akisaidiwa na Novatus Fulgence ambaye ni kocha msaidizi Patrick Mwangata - kocha wa makipa pia yumo Meneja wa timu, Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu, Daktari wa timu ni Richard Yomba na Daktari wa viungo ni Gilbert Kigadye ni makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar). Walinzi wa pembeni wako Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Kessy (Yanga SC), Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael.

Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) ilihali viungo wa kuzuia ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude kutoka Simba SC ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu baada ya kupata ajali.

Viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na Mzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa pembeni ni Simon Msuva (Yanga SC), Shizza Kichuya (Simba SC) na Farid Mussa (Teneriffe, Hispania). Washambuliaji wapo Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting).
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga (kulia) akikagua Uwanja ambao timu itautumia kwa ajili ya mazoezi kwenye kambi ya Tolip Sports City, Alexandia, Misri. Wengine ni kutoka kushoto Mkuu wa Msafara (HOD), Wilfred Kidao ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF, Meneja wa timu, Danny Msangi na Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Novatus Fulgence.

Madakatari na lishe :Madaktari wa Taifa Stars, Dk. Gilbert Kigadye (aliyesimama kushoto) na Dk. Richard Yomba (aliyesimama kulia) wakitoa maelekezo ya chakula hitajika kwa baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars.

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga (kulia) na viongozi wengine wakikagua ukumbi wa mazoezi ya viungo ‘Gym’.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad