HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 21, 2017

Sumaye ajiuzulu ujumbe wa bodi CRDB

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye amejitoa katika Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB kwa madai kuwa familia yake inafuatwafuatwa hivyo kuhofia kuwa anaweza kuathiri benki hiyo.

Baada ya kujitoa kama mmoja wa viongozi wa benki hiyo kubwa nchini, Sumaye amesema kuwa ataendelea kuwa mwanahisa wa benki hiyo ya biashara.

“Sitaki msimamo wangu wa kisiasa uhusishwe na benki yetu” alisema Sumaye ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani.

Sumaye alisema kuwa huenda majukumu yake ya kisiasa yakambana na akashindwa kuhudhuria baadhi ya vikao muhimu vya benki hiyo ambavyo ni muhimu kwa ufanisi na ustawi wa benki.

Akiwa nje ya mkutano huo Sumaye alisema kuwa, familia yake imekuwa ikifuatwafuatwa na serikali na kwamba tayari mtoto wake amepokwa shamba.

Serikali pia alimnyang’anya Sumaye shamba lake lililokuwa Mabwepande kwa madai hakuliendeleza, huku yeye akisema uamuzi wa yeye kupokwa shamba ulikuwa ni wa kisiasa. Sumaye alieleza kwamba hakuweza kulima shamba hilo kutokana na serikali kupiga kilimo jijini Dar es Salaam.

Sumaye amesema uamuzi wake aliuchukua ili CRDB iweze kuendeshwa na watu walioko huru mbele ya jamii kuepusha hisa za wafanyabishara wengine kuathiriwa.

Sumaye anamiliki zaidi ya hisa milioni 7.4 za benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad