HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 1, 2017

STAMICO WASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI, WAAHIDI KUCHAPA KAZI KUCHANGIA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI

Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) leo wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyoadhimishwa kimkoa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo waliahidi kuchapa kazi ili kuchangia maendeleo ya Viwanda kupitia miradi ya uchimbaji madini inayotekelezwa na Shirika hilo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika hafla ya maadhimisho hayo jijini, Makamu Mwenyekiti Chama cha Wafanyakazi wa Migodi, Nishati, Ujenzi na Huduma zingine, tawi la STAMICO (TAMICO) Bwana Denis Silasi, amesema wafanyakazi wa STAMICO ni muhimili mkuu katika kuwezesha viwanda kujiletea maendeleo kwa kupitia miradi mbalimbali ya madini yanayozalisha madini yakiwemo Makaa ya Mawe, Graphite, Tanzanite, Dhahabu, Madini ya viwandani na mengineyo ambayo pia hutumiwa na wenye viwanda katika uzalishaji.

“kama kauli mbiu inavyoelezea uchumi wa viwanda uendane na kulinda Haki na heshima ya mfanyakazi, TAMICO kwa kushirikiana na Menejimenti ya STAMICO itaendelea kulinda haki za watumishi na kutetea maslahi yao ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na motisha ya kufanya kazi wakati wote kwa manufaa na Shirika na Taifa kwa ujumla na hivyo kuiwezesha Tanzania kuwa Tanzania ya Viwanda.” Alifafanua Bwana Silasi.

Amewataka Watumishi wa STAMICO kutumia utaalam, ujuzi na weledi wao katika kutekeleza miradi mbalimbali ya uchimbaji madini inayotekelezwa na Shirika katika maeneo mbalimbali nchini.    
                                                                 
“Watanzania wanategemea sana ujuzi na utaalam wa watumishi wa STAMICO ili kuboresha hali zao za uchumi kupitia shughuli za uchimbaji madini, hususani katika miradi ambayo inatekelezwa na STAMICO moja kwa moja au ile ya ubia” Alisisitiza Makamu huyo Mwenyekiti wa TAMICO-STAMICO Bwana Silasi.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kwa mkoa wa Dar es Salaam alikuwa Rais Mstaafu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bi.Magreth Sitta.
     Makamu Mwenyekiti Chama cha Wafanyakazi wa Migodi, Nishati, Ujenzi na Huduma zingine, tawi la STAMICO (TAMICO) Bwana Dennis Silasi, (wa kwanza kushoto aliyeshilia bango) akiwa nje ya uwanja wa Uhuru na timu ya wafanyakazi wa STAMICO wakijiandaa kuingia uwanjani kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2017 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa STAMICO wakijiandaa kuingia ndani ya uwanja wa uhuru kushiriki katika maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa mkoa wa Dar es Salaam leo
Wafanyakazi wa STAMICO Bi. Ndumbula Msaki (aliyeshika bango kushoto) na Rose Ngowi  (aliyeshika bango kulia) wakijiandaa kuingia ndani ya uwanja wa Uhuru kushiriki katika maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyoadhimishwa katika uwanja huo katika ngazi ya mkoa.

Wafanyakazi wa STAMICO wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya uwanja wa uhuru mara baada ya baada ya kumalizika kwa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambampo kimkoa wa Dar es Salaam zilifanyika kwenye uwanja wa uhuru.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad