HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 22, 2017

SOMO MTANDAO: KUENDELEA KUKUA KWA UHALIFU MTANDAO - NANI WA KULAUMIWA?

Kumeendelea kukua kwa uhalifu mtandao maeneo mengi duniani – Huku baadhi wakitafsiri hili linatokana na wana usalama mtandao kuonekana kulemewa (Kuzidiwa) na wahalifu mtandao.

Hili limepingwa katika kikao kilicho kamilika mwishoni mwa wiki iliyopita, Nchini Afrika kusini ambapo binafsi nilishiriki na kuzungumza na wenzangu kuhusiana na namna sahihi ya uchunguzi wa makosa ya kimtandao – Kubwa nililozungumzia ilikua ni kuwa rudisha wenzangu kwenye mstari kwa kuwakumbusha juu ya taratibu tulizojiwekea na zinazo takiwa kufatwa na mataifa yote duniani.

Pamoja na mambo mengine, nilikumbusha umuhimu kuhakiki hatua zote za uchunguzi zinakua katika maandishi – Zaidi, nilicho zungumza pia kinaweza kupatikana katika Habari inayoweza kusomeka “HAPA”

Kuhusiana na ukuwaji wa uhalifu mtandao kila mmoja wetu amekiri hili halisababishwi na wana usalama mtandao kuzidiwa nguvu – Lawama imeonekana kuelekezwa kwa mataifa mbali mbali pamoja na watumiaji wa mwisho “Users”.

Lawama kwa mataifa mbali mbali – Kila uhalifu mtandao unao jitokeza leo umekua ukitabiriwa kabla na mapendekezo kutolewa na wana usalama mtandao isipokua tu kwa matukio machache sana mfamo, Tukio la ModPOS.

Mataifa kupitia vitengo vyake vya kukabiliana na uhalifu mtandao vilipaswa kufatilia maangalizo na maelekezo yanayo tolewa bahati mbaya sana mataifa mengi yamekua hayatekelezi hili. Mara zote baada yatatizo lililotabiriwa na kutolewa ufafanuzi kujitokeza ndipo vitengo husika katika mataifa vitaonekana kutahadharisha wananchi wake kitu ambacho wana usalama mtandao tumekubaliana hatua hii ya “Fire fighting” Kuangaika na tatizo baada ya kutokea ndio hasa sababu ya kuendelea kukua kwa uhalifu mtandao.

Tukio la hivi karibuni la uhalifu mtandao aina ya Ransomware ambao kimsingi umedumu kwa muda mrefu na maangalizo yalisha tolewa umetumika kama mfano – Atahri za uhalifu huu (WanaCry) inaweza kuonekana kwenye video hapa chini.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad