HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 21 May 2017

RAIS DONALD TRUMP KUOMBA KUUNGWA MKONO VITA DHIDI YA IS

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuelezea umuhimu wa kukabiliana na itikadi kali katika Uislam wakati akitoa hotuba yake nchini Saudi Arabia baadaye hii leo.

Hotuba yake hiyo katika mkutano wa viongozi wa dini, anatoa ikiwa ni katika siku yake ya pili katika ziara yake ya kwanza nje ya Marekani tangu awe rais.

Inaelezwa kuwa atajaribu kufanikisha makubaliano ya ushirikiano wa kuimarisha kuungwa mkono Marekani katika vita dhidi ya wapiganaji wa kundi la Dola ya Kiislam (IS).

Hapo jana Marekani ilitia saini makubaliano ya kibiashara yenye thamani ya dola bilioni 350 na Saudi Arabia.
                 Rais Donald Trump akiwa na mwenyeji wake Mfalme Salman wa Saudi Arabia

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad