HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 2 May 2017

NMB yapata taarifa bora za hesabu

• Yapata faida ya shilingi bilioni 40.9 kwa miezi Mitatu 
 • Ni ongezeko la asilimia 4 

BENKI ya NMB imepatafaida ya shilingi Bilioni 40.9 kwa miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka ikiwa ni ongezeko la 4% ya faida ukilinganisha na kipindi kama hicho Mwaka jana – 2016 ambapo NMB ilipata faida ya shilingi Bilioni 39.3. Mkurugenzi wa Benki ya NMB - Ineke Bussemaker alisema mwanzo huu wa Mwaka mzuri katika faida ya benki umetokana na kuimarika kwa pato linalotokana na biashara ya benki na ahueni iliyopatikana katika mikopo mibovu au isiyolipika. 

Bi Bussemaker alisema pato linalotokana na biashara ya benki lilikua kwa asilimia 4.6 hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 58.7 ikilinganishwa na kiasi cha bilioni 56.1 zilizopatikana katika kipindi kama hicho mwaka jana. 
 Mkurugenzi wa Benki ya NMB - Ineke Bussemaker

Alisema ongezeko hili limechangiwa kwa kiasi kikubwa na pato linalotokana na riba katika mikopo na biashara ya fedha za kigeni ambalo limeongezeka kwa asilimia 41 hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 4.9 katika robo ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na shilingi bilioni 3.5 zilizopatikana katika kipindi kama hicho mwaka jana.

 “Robo ya kwanza ya mwaka 2017, pato linalotokana na riba katika mikopo ilikuwa shilingi za kitanzania bilioni 115.9, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.4 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi bilioni106.0 katika kipindi kama hicho mwaka jana na pia ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.9 hadi shilingi bilioni 114.9 katika robo ya mwisho ya mwaka 2016,” alisema Bi Bussemaker. 

Pia taarifa hii ya hesabu za benki inaonyesha kuwa pato lisilotokana na riba katika mikopo limeongezeka kwa asilimia 5.3 hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 41.5 katika robo ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na kiasi cha shilingi bilioni 39.4 katika kipindi kama hicho mwaka jana na pia ikilinganishwa na ongezeko la asilimia nne kutoka shilingi bilioni 39.9 katika robo ya nne ya mwaka 2016. 

Amana za wateja nazo ziliongezeka kwa asilimia 0.9 hadi kufikia shilingi trilioni 3.75 katika robo ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.71 katika robo ya mwisho ya mwaka jana. “Ili kuongeza idadi ya wateja na amana, benki imeweza kutumia zaidi NMB wakala, walioponchi nzima. Lengo la benki ni kuwa na mawakala wapatao 4,500 mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu," alisema Bi Bussemaker 

Bi Bussemaker pia alisema katika kupambana na changamoto ya ukata katika soko, benki imeweza kuongeza umakini katika kutoa mikopo kwa Wateja. Mikopo iliyotolewa kwa Wateja katika robo ya kwanza yam waka ilipungua kwa 1.2% mpaka kufikia shilingi trilioni 2.76 kutoka shilingi trilioni 2.79 zilizonukuliwa katika robo iliyopita. Uwiano wa mikopo na amana za NMB umeendelea kuwa mzuri kwa Kiwango cha 74.6%, ukusanyaji wa mikopo inadhihirishwa na Kiwango cha mikopo mibaya au isiyolipika ambacho kimepungua mpaka kufikia 4.6% kutoka 4.8% iliyopatikana mwaka jana. 

“Menejimenti imedhamiria kuendelea kutoa hesabu nzuri na mwisho wa siku kuleta matunda kwa wana hisa wa benki ya NMB kwa mwaka 2017,” alisema Bi Bussemaker. Kuhusu NMB: NMB ni benki inayoongoza nchini Tanzania kwa matawi, ikiwa na zaidi ya matawi 189, wateja zaidi ya milioni 2 na laki tano na zaidi ya mashine 700 za kutolea fedha (ATM) nchi nzima. 

NMB imeasisi ubunifu mkubwa katika soko la Tanzania ikiwa ni pamoja na huduma za benki kwa njia ya simu yaani NMB mobile , Pesa Fasta na malipo kwa kutumia mashine za ATM. NMB inaendelea kujikita katika kutoa huduma kwa makampuni makubwa, masoko ya kifedha pamoja na huduma za kusaidia makusanyo ya kifedha na biashara. Lakini Pia imekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya kilimo na imeanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia vyama vya ushirika nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad