HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 27, 2017

NAIBU WAZIRI NGONYANI AKAGUA UJENZI DARAJA LA KELEMA

 Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akikagua hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari.
 Mkandarasi wa Kampuni ya Chicco, Li Jianzheng, akimounesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kulia), namna ya usukwaji nondo katika Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220 wakati alipokagua daraja hilo mkoani Dodoma leo.
 Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu ujenzi wa Daraja la Msui lenye urefu wa mita 45 lililopo katika barabara hiyo, mkoani Dodoma, leo.
 Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mela – Bonga Km 88.8 Eng. Kini Kuyonza akimuonesha taarifa ya mradi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wakati alipokuwa akikagua barabara hiyo, mkoani Manyara, leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akikagua zege lililowekwa katika barabara ya Mela-Bonga KM 88.8 eneo la Mlima Kolo uliopo wilaya ya Kondoa, wakati alipokagua ujenzi wake, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Kini Kuyonza

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Akizungumza leo mkoani Dodoma, mara baada ya kukagua daraja hilo lililopo katika barabara ya Mayamaya-Mela KM 99.35, Naibu Waziri Ngonyani  amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo na  barabara za maingilio katika daraja hilo kutarahisisha  huduma ya usafiri kwa wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani ya  Manyara na Arusha.
"Daraja hili na barabara zake ni kiungo muhimu kati ya mkoa huu na mikoa  ya Manyara na Arusha  na pia inaunganisha  nchi ya Tanzania, (Cape Town) South Afrika hadi (Cairo) Misri, hivyo kurahisisha huduma za  usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka hapa kuelekea maeneo mengine", amesema Eng.Ngonyani.
Aidha, Naibu Waziri ameitaka kampuni ya ujenzi ya Chico kuhakikisha inamaliza daraja hilo ifikapo mwezi wa Kumi mwaka huu kama ilivyoandikwa kwenye mkataba ili wananchi kuweza kulitumia.
Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa mradi huo, Eng. Leornado Licari, amesema kuwa kwa sasa mradi umefika asilimia 87 ambapo hivi karibuni wanatarajia kuweka lami.
"Nakuhakikishia kumaliza mradi huu kwa wakati kwani kazi zilizobaki kwa sasa hivi ni chache, kwa hiyo hadi kufikia mwezi Septemba tutakuwa tumeshakamilisha kazi zote", amesisitiza Mhandisi Mshauri Licari.
Naibu Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kikazi ya siku moja katika mikoa ya Dodoma na Manyara ambapo pamoja na ukaguzi wa daraja hilo pia amekagua madaraja mengine matatu likiwemo la Msui, Kingali na Mela pamoja na ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga KM 88.8.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad