HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 24 May 2017

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SARPCCO WAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati anawasili katika ukumbi wa mikutano wa AICC kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO). Kulia ni Mkuu wa INTERPOL kanda ya Kusini Mubita Nawa.
 Katibu Mtendaji wa SADC, Dk. Stegnomena Tax akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kabla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika mkoani Arusha. IGP Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki.
 Baadhi ya Wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika SADC wakitoa heshima wakati wimbo wa taifa unapigwa wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) uliofanyika Mkoani Arusha. IGP wa Tanzania, Ernest Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki. 
 Katibu Mtendaji wa SADC, Dk.Stegnomena Taxi, akitoa hotuba wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni Mkoani Arusha. IGP wa Tanzania Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa afrika (SARPCCO) baada ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika unaofanyika Mkoani Arusha.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,  IGP Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwa ameambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Angola, Paulo de Almeida (kushoto) na Mkuu wa jeshi la Polisi la Msumbiji, Paulo Chachine (kulia) wakati wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) uliofanyika Mkoani Arusha.(Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad