HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 11 May 2017

MISS TANZANIA AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA GARI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kamati ya Miss Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Grace Product na Gift Jewelers wamekabidhi gari kwa Mrembo wa Shindano hilo Diana Edward Lukumai  ambaye alishinda taji la Miss Tanzania 2016/2017.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa zawadi hiyo Miss Diana amesema kuwa  anaishukuru sana kamati hiyo kwa kumsaidia kupata zawadi hiyo ambayo ameisubiri kwa hamu na kwa muda mrefu .

“Wasichana wanatakiwa kuwa wavumilivu na kujiandaa kisaikolojia kwani kushinda taji la urembo la Miss Tanzania sio kitu kidogo, watu wengi watakufuatilia, hivyo lazima ujitambue kuwa ukiwa Miss Tanzania ni mtu ambaye anatakiwa kuwa msiri,  hivyo wasichana wajiandae sana kisaikolojia katika hili.” Amesema Miss Diana.

Amesema kuwa gari hiyo itaweza kumsaidia katika matumizi yake binafsi hasa katika kipindi hiki ambacho anaendelea na kampeni yake ya Dondosha wembe ambayo ina lengo la kumkomboa  mtoto wa kike juu ya mila potofu za kuozeshwa mapema na ukeketaji.

Kwa upande wake mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania, Albart Makoye amesema mara baada ya kukabidhi kwa zawadi hiyo kunafungua pazia la shindano jipya la mwaka 2017/2018 .

Amesema kuwa warembo wanatakiwa kujiweka sawa hili waweze kunyakuwa taji hilo ambalo mashindano yake yataanza kuanzia ngazi ya votongoji mpaka taifa.
 Ofisa wa Basata akikabidhi funguo kwa Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai  kama ishara ya kumkabidhi mrembo  huyo gari yake aina ya Suzuki Swift pembeni yake Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili.
 Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai akiingia ndani ya gari yake mara baada ya kukabidhiwa
 Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai akifurahi mara baada ya kuingia ndani ya gari yake
 Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania , Arbart Makoye akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi gari
 Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili na Mumewe  wakikabidhi kadi ya gari kwa Miss Tanzania 2016/217 Diana Lukumai
 Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili. akizungumza na Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai katika duka la ke lililopo City Mall jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad