HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 20, 2017

MECHI ZOTE ZA MWISHO VPL KUANZA SAA 10.00 JIONI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tunafahamisha kuwa mechi za mwisho za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 zitachezwa kuanzia saa 10.00 jioni bila kujali kama jua linawahi au kuchelewa kuzama. Muda huo umepangwa ili kuhakikisha timu zote zinamaliza mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinamalizika siku moja ya Mei 20, mwaka huu na kwa muda mmoja, ikiwa ni pamoja na kudhibiti viashiria vyo vyote vya upangaji wa matokeo. Ni jukumu la kila kamishna kuhakikisha mechi anayosimamia inaanza katika muda ulipangwa bila kujali kama kuna mgeni rasmi au la. 

TAIFA STARS MPYA HII HAPA Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania, Salum Mayanga leo Ijumaa Machi 19, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 24 watakaounda kikosi hicho cha Timu ya Taifa Stars ambacho sasa kinachodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti. Katika mkutano na wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya TFF, yaliyoko Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, Mayanga alisema kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar). Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Haji Mwinyi (Yanga SC). Mayanga aliwataja walinzi wa kati Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Aggrey Morris (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC). Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na Muzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba SC). Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting).

Pia Mayanga aliwataja wasaidizi wake kuwa ni Kocha Msaidizi kuwa ni Novatus Fulgence wakati Kocha wa Makipa, Patrick Mwangata wakati Meneja wa atakuwa Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu wakati Daktari wa timu atakuwa Richard Yomba huku Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.
Timu hiyo itaingia kambini Machi 23, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam mpaka tarehe 29 baada ya hapo itasafiri kwenda Misri kwa kambi ya wiki moja kabla ya kurejea kuja kucheza mchezo wa kufuzu Mataifa huru ya Afrika mchezo na Lesotho, mchezo utachezwa Tarehe 10 mwezi wa 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam. 


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad