HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 24 May 2017

Mchezo wa m-Bet wamwaga shilingi milioni 826

Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Kabora Mboya(kushoto)akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 109/- Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa,Raymond Bintabara,aliyejishindia kupitia mchezo wa kubahatisha wa Supper 12 unaoendeshwa na M-bet,hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es salaam,Wanaoshuhudia wapili kushoto ni Msemaji wa M bet,Godluck Wambura na Meneja wa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo, Jaykishan Kaba. 
Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Kabora Mboya(kushoto) Msemaji wa M bet,Godluck Wambura wakimsikiliza kwa makini mshindi wa shilingi milioni 109/- Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa,Raymond Bintabara(26)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ya kumkabidhi mshindi huyo hundi yake aliyojishindia kupitia mchezo wa kubahatisha wa Supper 12 unaoendeshwa na M-bet.
Meneja huduma kwa wateja wa M bet, Jaykishan Kaba na Msemaji mkuu wa kampuni hiyo,Godluck Wambura wakimwelekeza mshindi wa shilingi milioni 109/- ambaye ni Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa,Raymond Bintabara jinsi ya kujaza fomu za kuwekewa fedha zake kwenye akaunti yake wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi mshindi huyo hundi yake aliyojishindia kupitia mchezo wa kubahatisha wa Supper 12 unaoendeshwa na M-bet.
Watanzania elfu 22 wamefanikiwa kujishindia jumla ya shingi milioni 826 kupitia mchezo wa kubashiri matokeo ya mechi za ligi za Ulaya m-Bet.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa kumkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 109,388,350/- Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Iringa  Raymond Bintabara (26) aliyeibuka mshindi wa kitita hicho, Msemaji wa M bet,Godluck Wambura  aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa, kampuni yake itaendeleo kutoa zawadi kwa washiriki wanaofanya vizuri katika utabiri wa motokeo ya mechi.

Mpaka kufikia leo hii tumeshatoa zaidi ya shilingi milioni 826 na tuataendelea kutoa zaidi. Tunawashauri Watanzania kuchangamkia fursa  kwa kubashiri zaidi,” alisema 

Raymond Bintabara (26)  aliibuka mshindi baada ya kufanikiwa kubashiri kwa usahihi matokeo ya mechi 12 kupitia perfect 12 ya m-Bet

Akiwa mwenye furaha, Bintabara alikabidhiwa kitita hicho cha fedha katika hafla fupi iyofanyika katika ofisi za m-Bet zilizopo jijini Dar es Salaam.

“Leo tunayofuraha kubwa kumkabidhi Bintabara kitita hiki cha Sh milioni 109,388,350/- kwa kuwa mshindi wetu wa m-Bet. Tunaamini fedha alizoshinda zitamsaidia katika elimu yake lakini pia kwenye mambo mengine kwa ajili ya maendeleo yake”,  alisema mkurugenzi wa m-Bet.

Wambura aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa kwa kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Perfect 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote  unaondoka na kitita chako mchana kweupe na ndicho Bintabara alichofanya.

Kwa upande wake msindi wa siku aliwashauri watanzania wote pamoja na wanafunzi wenye umri unaoruhusiwa kisheria kujitokeza kubashiri matokeo ya mechi mbalimbali kupitia Kampuni ya m-Bet ili kujishindia mamilioni.

"Nashukuru sana m-Bet, nitatumia fedha hizi kutimiza ndoto zangu za kielimu pamoja na za kimaisha kwa ujumla", alisema.

m-Bet, ni Kampuni iliyosajiliwa chini ya Sheria za Tanzania na kupewa leseni na Bodi ya Michezo ya kubahatisha tanzania kwa lengo la kufanya upatikanaji rahisi na mwingiliano wa huduma ya mchezo wa kubahatisha (Sim Betting) nchi nzima

“Kushiriki, ingia www.m-bet.co.tz, chagua kucheza kawaida au Perfect 12 ambapo kwa Shilingi 1000, unachagua matokeo 12. Ukipata yote sawa, unanyakua kikapu cha m-Bet,” alisema Kabba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad