Aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kumshambulia askari polisi.
Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi.
Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono amedai, Mei 15 mwaka huu huko
Masaki katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Malima
alitenda kosa.
Imedaiwa, siku hiyo mshtakiwa Malima alimzuia
afisa wa polisi mwenye namba H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake ya
kumkamata dereva wake Kigwande aliyekuwa amefanya kosa la kumjeruhi
Joseph Mwita ambaye ni afisa operation wa Priscane Business Enterprises.
Kombakono
ameongeza kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa Kigwande kwa nia ya
kukataa kukamatwa, alimjeruhi afisa operation hiyo(Joseph Mwita) ambaye
alikuwa anakamatwa kwa kosa la kupaki gari vibaya na kumsababishia Mwita
Majeraha Mwilini.
Watuhumiwa wote wamekana kutenda makosa hayo
na wako nje kwa dhamana.mahakama imemtaka kila mshtakiwa kuwa na
mdhamini mmoja atakaye saini dhamana ya milioni 5. Aidha Mahakama
imemtaka kila mdhamini awe na barua ya utambulisho kutoka ofisi yoyote
inayotambulika.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 15, mwaka huu
ambapo kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado
haujakamilika.Wakili Kibatala ameieleza mahakama kuwa, tarehe ya kutajwa
kwa kesi hiyo atawasilisha pingamizi la awali juu ya mapungufu ya
kisheria yaliyopo kwenye shtaka la shambulio linalomkabili Malima Peke
yake.
No comments:
Post a Comment