HABARI MPYA

Home Top Ad



Post Top Ad

Monday, 15 May 2017

MADEREVA HIACE WAGOMA, WAKIMBILIA PORINI WAKIDAI BORA WAFIE HUKO MKOANI SONGWE LEO....

Madereva wa haisi zinazofanya safari za Tunduma kwenda Mlowo wamegoma kutoa huduma hiyo kwa kile kinacholalamikiwa kuwa Askari  wa Usalama barabarani wamekuwa wakiwatoza faini nyingi pasipo sababu za msingi na wakati mwingine, faini hizo wanazolipa hawapewi lisiti .sambamba nahilo pia madereva hao wamedai wananyanyaswa wanataka waonane na mkuu wa mkoa wa songwe mheshimiwa Chiku Galawa iliwatoe kero zao.
Wakiongea katika mahojiano maalumu kiongozi wa madereva hao Ndugu Mgwalizi (Jina maarufu) kwasasa wanamsubili Mkuu wa Mkoa Mhe. Chiku Galawa katika eneo la Mpemba ndipo madereva hao walipo kwa sasa.
Kutokana na hali hiyo, Madereva hao wameamua kwenda nje ya Mji wa Tunduma, wakidai bora wakae porini na hata kufia huko kwani hawajasikilizwa kero zao. 
Baadhi ya madereva wa Mabasi ya mzunguko yafanyayo safari zake za kutoka Tunduma kwenda Mlowo wakiwa katika eneo walilokusanyikia kwa pamoja kwa madai mbalimbali ikiwemo kusikilizwa kero zao.
Madereva Hiace wakiwa Wamejishika Vichwa na wengine tama (shavu) wakionyesha masikitiko yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad