HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 3 May 2017

KONGAMANO KUBWA LA AFYA KWA WOTE KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

WADAU wa sekta ya afya, watafiti, wanazuoni na wataalamu wa masuala ya bima, wanakutana jijini Dar es salaam kesho tarehe 4 Mei, 2017 kujadili suala la Afya bora kwa wote katika kongamano litakalofanyika katika hoteli ya bahari beach jijini dar es salaam.

Kongamano hilo kubwa kufanyika nchini linafanyika chini ya mwavuli wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (Public Private Partnership) linafanyika katika kipindi ambacho taifa linajiandaa kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu kupitia bima ya afya.

Mmoja wa waandaji wa kongamano hilo Dk. Heri Marwa kutoka Shirika la PharmAcess amesema kuwa jumla ya washiriki 250 kutoka makundi mbalimbali ya kijamii, utendaji na usimamizi na wawakilishi kutoka Serikalini wanatazamiwa kushiriki. Kongamano hilo limeandaliwa kwa pamoja kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) na Shirika la PharmAccess linalosimamia huduma ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa katika mikoa ya Kilimanjaro na Manyara kazi ambayo PharmAcess wanafanya kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika mikoa hiyo.

Kwa mujibu wa Dk. Heri lengo la kongamano hilo ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali kuelekea afya bora kwa wote na umuhimu wa wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo. Amesema pia washiriki watapata fursa kubadilisha uzoefu katika maeneo muhimu ambayo ndio dira kuu ya kuelekea afya bora kwa wote yanayohusu; kuongeza uwigo kwa makundi mbalimbali hasa sekta isiyo rasmi, umuhimu wa huduma bora na masuala ya TEHAMA pamoja umuhimu wa masuala ya utafiti.

Nchi mbalimbali hasa barani Afrika zimekuwa zikikwama kutekeleza azma hii kutokana na kukosekana kwa utashi wa kisiasa. Bahati njema hapa nchini suala hili lina utashi mkubwa wa kisiasa. Kazi kubwa katika kongamano hili itakuwa ni kubaini matarajio na changamoto na kueneza mifano bora (best practises) inayotekelezeka wakati tukielekea kutekeleza azma hiyo ya afya kwa wote alimalizia Dk Heri na kuwakumbusha washiriki wote waliothibitisha kushiriki kuwahi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad