HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 22, 2017

KIVUKO CHA MV KAZI CHAANZA KUFANYIWA MAJARIBIO DAR

Kivuko cha MV KAZI kikielea kwa mara ya kwanza majini huku kikiwa na abiria na magari, kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
Na Alfred Mgweno, TEMESA 
 Kivuko cha MV KAZI hatimaye kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na magari kwa mara ya kwanza baada ya kukamilika kwa matengenezo yake. 
Majaribio hayo yalifanyika kulingana na sheria na taratibu za vyombo vya majini ambayo inavitaka vyombo vyote vya majini kufanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi ili viweze kupatiwa cheti cha ubora “Seaworthiness Certificate”.

Awali wataalam kutoka Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI) waliweza kupima ubora na uimara wa kivuko hicho kwa kutumia utaratibu wa kuweka mawe yenye kilo zinazolingana na uwezo wa kivuko pamoja na magunia ya mchanga ili kuweza kupima uwezo wa kivuko kulingana na mahitaji yaliyoainishwa kabla hakijabeba abiria na mizigo. 

Zoezi hili pia lilihusu kufanyika kwa kipimo cha kuhakikisha kuwa kivuko hakilali upande mmoja yaani “Inclination test” ambapo kilionyesha Kivuko kiko sawa. Taarifa ya zoezi hili itakuwa sehemu ya vitu vya makabidhiano wakati wa upokeaji wa Kivuko.

Miongoni mwa waliokuwepo kushuhudia majaribio hayo alikuwa Mkuu wa Vivuko Magogoni/Kigamboni, Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alisifu uwezo wa kivuko hicho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanakitunza kivuko hicho kwani kitawasaidia kupunguza msongamano wa abiria na magari hasa majira ya asubuhi na jioni.Ujenzi wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170. 

Kivuko hicho kitakabidhiwa rasmi hivi karibuni kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kuanza kutoa huduma. Aidha ujio wa kivuko hicho utaongeza idadi ya vivuko kufikia vitatu vitakavyotoa huduma ya kuvusha abiria na magari katika eneo la Magogoni/Kigamboni.
Abiria wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
Abiria wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
Kivuko kipya cha MV KAZI kikiwasili kwa mara ya kwanza upande wa Magogoni tayari kwa majaribio ya kubeba abiria na magari. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad