HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 15, 2017

Jokate awaomba watu maarufu kusaidia kuondoa changamoto katika sekta mbalimbali nchini

Mwanamitindo, muigizaji  na Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo ametoa wito kwa watu maarufu nchini kusaidia kuondoa changamoto katika sekta mbalimbali ili kupunguza mzigo kwa serikali. Jokate alisema hayo wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani ambapo jumla ya wanafunzi 118 walihitimu katika shule hiyo.

Mrembo huyo ambaye ni Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa  Umoja wa Vijana  wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) amesema kuwa Tanzania ina watu wengi maarufu na wenye uwezo, lakini wachache tu ndiyo wamekuwa wakijitolea kusaidia sekta mbalimbali husasani elimu na afya.
Miss Tanzania namba mbili 2006 na Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo akikabidhi cheti kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza mtihani wao. 

Alisema kuwa kwa hali ilivyosasa, ni vigumu kwa serikali kutatua matatizo yote na kuwaomba  wanamuziki, wasanii, wafanyabiashara na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali kujitolea kusaidia kutatua matatizo katika jamii.

Alifafanua kuwa shule ya wasichana ya Jangwani ni kongwe  kutokana na kuanzishwa Mei 28, 1928, lakini mpaka sasa inakabiliwa na matatizo mbalimbali wakati kuna wahitimu wengi ambao kwa sasa wana nyandhifa na wanashindwa kuchangia.

“Mimi sijasoma Jangwani, lakini niliguswa na matatizo ya viwanja vya michezo na kuamua kujenga uwanja wa mpira wa kikapu na mpira wa pete (netiboli), nashukuru viwanja kwa sasa vinatumiwa na shule zinazozunguka maeneo haya,naomba wengine wasaidie, kuondoa changamoto zilizopo,” alisema Jokate.

Mrembo huyo pia amewaomba viongozi wa serikali na wafanyabiashara  waliosoma katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Jangwani, kusaidia kuondoa changamoto za shule hiyo.

Awali, Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Amos Mgongolwa alisema mbali ya uchakavu wa majengo, shule yao haina madarasa na mabweni ya kutosha, haina  ukumbi wa kufanyia shughuli mbalimbali kama sherehe na kulazimika kufanyia eneo la wazi, shule haina hata gari moja kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na matibabu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Mgongolwa amesema wanafunzi wenye mahitaji maalum, ulazimika kutumia baiskeli za miguu mitatu ili kwenda  kwenye shughuli mbalimbali za kimamoso nje ya shule.
Miss Tanzania namba mbili 2006 na Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza mtihani wao.
Kaimu Mkuu wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa akizungumza katika mahafali hayo.
Jokate Mwegelo akizungumza katika mahafali hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad