HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 29 May 2017

JIMBO LA PUNTLAND SOMALIA LAPIGWA 'TAFU' KUBORESHA UTUMISHI WA UMMA


Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki (kulia) akibadilishana mkataba wa ushirikiano wa kuboresha sekta ya utumishi wa umma jimboni Puntland na Waziri wa Kazi,Vijana na Michezo wa Puntland Abdurahman Ahmed Abdulle, serikali kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Puntland itaendesha mafunzo hayo. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Puntland Mahmood Hamad.Hafla ilifanyika mwishoni mwa wiki (Picha zote na Ino Communications)
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki (Kulia) na Waziri wa Kazi,Vijana na Michezo wa Puntland Abdurahman Ahmed Abdulle wakisaini mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano wa kuboresha sekta ya utumishi wa umma jimboni Puntland ambapo serikali kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) itaendesha mafunzo hayo kwa kushiriakana na Chuo Kikuu cha Puntland. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Puntland Mahmood Hamad.

Mashauri wa kisheria kutoka Puntland Burhan Adam Omar akijadili jambo kabla ya kutia saini makubaliano baina ya Tanzania na Jimbo la Puntland makubaliano ya ushirikiano wa kuboresha sekta ya utumishi wa umma jimboni Puntland ambapo serikali kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) itaendesha mafunzo hayo kwa kushiriakana na Chuo Kikuu cha Puntland.
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja , katikati ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki, wa Kwanza kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Puntland Mahmood Hamad, wa Pili Kushoto ni Waziri wa Kazi,Vijana na Michezo wa Puntland Abdurahman Ahmed Abdulle,Wanne kushoto ni Mkuu wa TPSC Dk. Henry Mambo na wa kwanza kulia ni Mustapha Said Shaba Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Puntland.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad