HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 6 May 2017

ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE: ZAIDI YA WANAFUNZI 20 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI HUKO KARATU ASUBUHI HII

Taarifa iliyotufikia hivi punde, kuna ajali imetokea muda huu katika eneo la Rhotia Wilaya ya  Karatu Mkoani Arusha, iliyohusisha Basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St Lucky ya jijini Arusha, inayodaiwa kuwa ilipoteza mueleo na kupinduka wakati wakiwa safarini kuelekea Karatu waliokuwa wakienda kufanya mitihani na wanafunzi wenzao wa Shule ya Tumaini English Medium ya Karatu. Inadaiwa kuwa wanafunzi zaidi ya kumi na walimu wao wamepoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa. jitihada za kumtafunda Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara zinaendea ili kupata kauli yake juu ya ajali hii. Pichani ni baadhi ya wasamalia wakitoa msaada wa uokozi kwa wanafunzi hao.
Zoezi la uokoaji kwa wanafunzi hao likiendelea. 
Zoezi la uokoaji likiendelea. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad